Wapendwa
Wana-LEKIDEA, na Wapenda Maendeleo wote wazaliwa wa Ukanda wa
Legho-Kirua Vunjo Mashariki, na Wapenda maendeleo wote popote walipo
Tanzania na Dunia Nzima. Salaam ziwafikie!
Uongozi
wa Taasisi yetu muhimu ya Legho-Kirua Develeopment Association
(LEKIDEA), hivi karibuni (22/07/2012) ulifanya Kikao Muhimu cha
kufuatilia mambo muhimu na Utekelezaji wa Miradi iliyo katika Mikakati
na Malengo ya Taasisi hii muhimu inayolenga kunyanyua maisha ya Eneo
walilozaliwa la Legho-Kirua Vunjo Mashariki. Kikao kilikuwa cha manufaa
sana.
Pamoja na Mambo mengine muhimu, Kikao hiki kilichoongozwa na M/Kiti wa Taasisi Ndg Edward F. Msaky,
kilikuwa cha mafanikio makubwa, na kiliweza kujenga midani na mikakati
bora kabisa katika kuifanya Taasisi kutimiza malengo yake na majukumu
muhimu iliyojiwekea katika kuukomboa ukanda wetu katika hali ya
'kusahaulika' kimaendeleo na kiuchumi. Baadhai ya masuala muhimu
yaliyofanyiwa kazi ni pamoja na Kufuatilia kwa umakini Mradi wa
Ukarabati wa Barabara za Vijiji vyote vya Legho-Kirua Vunjo, (kama
ilivyoainishwa katika Taarifa Rasmi kwa Vyombo vya Habari 'Press
Release' chini) ambapo Mradi wenyewe ulishaanza.
Pia
mikakati mingine katika Kikao ilihusu uhamasishaji zaidi wa wazaliwa
wote wa maeneo ya Legho-Kirua Vunjo Mashariki popote walipo ili waweze
kuungana zaidi na kuchangia kwa hali na mali katika kuhakikisha
maendeleo yaliyokusudiwa kwa kupitia taasisi hii ya LEKIDEA inafanikiwa
kwa kiwango kikubwa ili kufaidisha wananchi wote wa sasa na vizazi
vijavyo.
Kadhalika,
suala muhimu la kuwafahamisha wanachama wote wa Legho-Kirua, Tanzania
nzima na wapenda maendeleo wote, hali halisi na maendeleo ya Michango ya
wanachama, Miradi na malengo ambayo yalikwishafikiwa hadi sasa, ili kwa
njia moja au nyingine waendelee kuhamasishana kila mwanachama na
kuutambua umuhimu wa kuunga mkono juhudi hizi za LEKIDEA, kadhalika na
taasisi za ndani na nje ya nchi ambazo zinathamini hatua na juhudi hizi
za maendeleo kwa ngazi ya chini (vijijini) zinazofanywa na LEKIDEA, na
juhudi zilizokwishafanyika hadi sasa, wapate kutuunga mkono na kuchangia
maendeleo yetu kwa hali na mali kwa kupitia Taasisi yetu hii Rasmi
iliyosajiliwa kwa malengo na dhamira ya kuukomboa ukanda wetu kiuchumi,
kijamii na yote yanayohusika nayo. Dalili ni njema sana na yafaa
kutuunga mkono, na haraka tutasonga mbele zaidi.
Chini hapa ni baadhi ya Picha za matukio kadhaa muhimu zitokanazo na Kikao hicho:
Pichani: Toka kushoto, Makamu Katibu wa LEKIDEA Ndg Martin Kessy akifuatiwa na Ndg Emilian Saluo Assey na kulia kwake ni Ndg Amani-Ereney Kyara, wote wakisikiza na kufuatilia maendeleo ya kikao. |
-------------------&&&----------------------
WAPENDWA
WANA-LEKIDEA, NA WANANCHI WOTE WENYE MAPENZI MEMA YA KIMAENDELEO, HII
HAPA NDIYO TAARIFA RASMI YA LEKIDEA KAMA ILIVYOTOLEWA KATIKA GAZETI THE GUARDIAN LA TAREHE 03/08/2012.
MWANA-LEKIDEA,
TUENDELEE KUCHANGIA MAENDELEO YETU PASIPO KIKWAZO, AU KUKATISHWA TAMAA
NA MTU AU KIKUNDI CHOCHOTE, MAANA KUDHOOFU KWETU NDIO MTAJI KWA WENGINE,
NA TUJITAMBUE DAIMA KUWA MAENDELEO YETU YATALETWA NA SISI WENYEWE,
....NA WAKATI NDIO SASA!! TUUNGANISHE NGUVU!
No comments:
Post a Comment