LEGHO-KIRUA DEVELOPMENT ASSOCIATION
KIKAO CHA DHARURA CHA SEKRETARIAT NA UONGOZI WA LEKIDEA -26/10/2012
Double Views Hotel – Sinza DSM
KUTATHMINI HALI YA MAENDELEO YA BARABARA
------------------------------------------------------
Agenda
1.
Kufungua
Kikao
2.
Hali
ya Sasa – Current situation
3.
Hatua
zinzofuata - Way Forward
4.
Barabara
ndogo za Vitongoji - Periphery Roads
5.
Uzinduzi Rasmi wa Mradi
6.
Michango
7.
Mengineyo
------------------------------------------------------
1.
Kufungua
kikao
-Kikao kilifunguliwa saa 1:30 jioni kwa sala na Ndg.Joseph Shewiyo –
Katibu wa LEKIDEA.
2. Taarifa ya Hali ya Sasa toka KV.
Utangulizi:
-Mwenyekiti alianza kwa
kuwashukuru wajumbe wote ambao tangu kuanzishwa kwa LEKIDEA hadi sasa wamekua
wanajitoa kwa kila hali bila kuchoka na kuhakikisha miradi ya LEKIDEA inasonga
mbele bila kukwama hasa katika ujenzi wa barabara, ugumu wowote unaotokea wanabuni
mbinu mpya katika kukwamua. Aliwashukuru hususan Martin, Saluo, Shewiyo, Paul,
na pia ma-engineer Benin na Njau. Alimalizia kuwa Mungu awabariki sana kwa
uvumilivu na kujituma kwao kwa faida ya LEKIDEA na jamii nzima ya KV Mash.
3. Taarifa
Fupi toka KV:
Ø Martin
Kessy alitoa taarifa fupi ya hali ya uwekaji wa Moram iliyoanzia maeneo kadhaa
ya Mradi wetu kama ituatavyo:
·
Kiwelewele hadi kwa Matay.
·
Kisanja hadi Kisomachi
·
Kilasanioni hadi kwa Kikuyu-Kitaarinyi
·
Mrumeni hadi Kisomachi.
·
Pendekezo lilitolewa kujumuisha ya njia ya kuanzia
Kitaarinyi hadi Kisomachi
Ø Jumla
hadi siku ya kikao, idadi ya malori 200 yalikwishawekwa kwa gharama ya kiasi
cha sh.24,000,000 ila zimelipwa trip 100
tu imebaki deni trip 100 ambayo katika Mil 24 zilizopo sasa kiasi cha Mil 12
kitatumika kulipia hayo malori 100. Tutabakiwa na mil.12 ambazo zinatakiwa kufanya kazi ya
kusambaza, kumwagia maji na kushindilia. Aidha zinatakiwa pia kumalizia maeneo
matano muhimu ambayo ni barabara ya kutoka Uchira, Kitaarinyi hadi Kisomachi,
Kiwelewele hadi Mkombenyi, Kitaarinyi hadi kwa Erene na KNCU Usangi hadi
Kilasanioni
4. Hatua Inayofuata:
Ø Kutokana
na hali halisi, kiasi kilichosalia ni 12
mil. Michango zaidi inahitajika haraka ili kazi iendelee kwa kasi bila
kusimama.
Ø Zipo
trip kama 24 katika hizo mia mbili ambazo bado hazijawekwa. Imeshauriwa kuwa
tumkope mwenye Malori trip nyingine 50 ili zitoshe kuweka moram katika barabara
zifuatazo ambazo bado:
·
Kitaarinyi
kupitia Usangi hadi Kilasanioni.
·
KNCU hadi kwa-Rene
·
Kwelewele hadi Lasso - Juu (Mkombenyi)
·
Kitaarinyi hadi Kisomachi
·
Kisomachi hadi Uchira (pale Juu ya Maweni na
Kiorotsuni)
Ø Pia
imependekezwa kuwa Doza litengenezwe haraka ili kumalizia barabara za
KNCU hadi Kwa-Rene na KNCU hadi Usangi -Kilasanioni
Boza, Greda na Compactor:
Ø Imependekezwa
ipatikane haraka Boza, Greda na Compactor
kushindilia njia zote
zilizokwisha fanyika usambazaji wa Moram.
Ø Secretariet
itawasiliana na Wahandisi Ben na Njau walioko
KV ili kutathmin hali ya njia na maeneo ya
ndani watakayohitaji Culverts na ushauri
mwingine wowote ili kuimarisha kazi iliyokwishafanyika.
.
5. Barabara za Vitongoji – Periphery Roads
Ø Ufafanuzi
ulitolewa kuwa barabara zinazojengwa na Lekidea ni zile zilizoainishwa katika
mradi mkuu ambazo zinaunganisha vijiji vyote vya eneo hilo. Pia zile
zinazokwenda kwenye vyama vya ushirika vya msingi na mashule.
Ø Barabara
ndogo ziingiazo ndani ya vitongoji, zimewekwa kama ‘Peripheral roads’ za Lekidea
ambazo LEKIDEA haitaweza kufanyia kazi katika mradi huu mkuu bali familia
zinazotumia barabara hizo ndogo zikipenda
watachanga kwa ajili ya ukarabati wa njia hizo specific na LEKIDEA inaweza
kusaidia usimamizi zikatengenezwa ipasavyo. Hivyo ieleweke kuwa barabara
ndogo ndani ya vijiji au vitongoji, watachangia wahusika watumiaji wa njia hizo na LEKIDEA inaweza
kusimamia kazi husika.
6. Uzinduzi Rasmi
Ø Lilitolewa
pendekezo kuwa aombwe Kiongozi fulani afungue barabara zetu. Wazo hili
lilikubalika kwa kiasi ila litahitaji kupata maoni ya wajumbe wengine.
Ø Kutokana
na shughuli hii ya Uzinduzi kuwa muhimu sana, ilipendekezwa Ndg Venance Msaki
pamoja na Savinus Kessy watasaidia kuonana na Ndg Dennis Msacky (wa Mwananchi)
ili awezeshe kumwona Mgeni aliyependekezwa pindi tutakapo kubaliana katika
hatua hii. Mgeni rasmi huyo wa ufunguzi atakuwa muhimu kwetu katika suala zima
la Fund-Raising kwa ajili ya miradi
inayoendelea ambayo ni ya kufufua zao la Kahawa na kupanda miti na Mazingira.
Ø Pia
pendekezo la kumtumia Ndg Dennis Msacky kuweka Makala ya Miradi na majukumu ya
LEKIDEA katika gazeti la Mwananchi aliachiwa V. Msaki alifuatilie.
7. Michango.
Ø Martin
alitoa taarifa fupi ya michango
ambayo imeshaelezwa juu ni mil.24. Ukipunguza deni la trip 100 ambazo
ni sh.12,000,000, baki ni 12,000,000. Michango zaidi inatakiwa kuwezesha Moram
kuendelea.
Ø Taarifa ya Makusanyo na Matumizi hadi siku
ya Kikao
Taarifa kama ilivyowasilishwa
na Ndg Emilian Saluo ilikuwa kama ifuatavyo:
·
Makusanyo
Jumla ni Sh 65,866,626/-
·
Kiasi cha
hela haijaja ni 26,746,000.
·
Jumla ya
matumizi ni 42,860,410
·
Balance
kufikia leo 24,100,000
Kiasi kinachokuwa bado kinadaiwa
toka kwa wachangiaji ni 26,746,000 ambayo inatoka kwa waliokwisha ahidi, fedha ambayo
inahitajika kukusanywa mapema sana ili kumaliza kazi iliyosalia. Ilionekana
kuwa hawa walioahidi na bado kutoa fedha wanakwamisha malengo yetu. Imekubalika
kwa majina yote yachujwe yatangazwe kwa
jamii yetu. Iliafikiwa kuwa majina hayo
yawasilishwe kwa Bw Njau ili
awasilishe kwa Paroko ayatangaze
kanisani ili jamii iwatambue wagumu hao.
8. Mengineyo.
Ø Michango iendelee kuhamasishwa kwa SMS
, hii iliafikiwa kuwa iwepo njia ya
kutuma SMS kwa kila mdau. Uwepo muda
fulan ambapo kikao kikiafiki fedha kiasi
zitatoka kulipia central-SMS ambayo atatumia Paul Msaki kusambaza SMS kwa mtandao, Secretariet itajadili.
Ø Pia
ilipendekezwa kuwa sms fupi na nzuri
iandaliwe itumwe kwa wote hasa wale ambao wanagoma, ili angalau watoe kiasi chochote na
kila apataye SMS hiyo aisambaze pia kwa wengine .
Kikao kilifungwa saa 3:15 usiku kwa sala
Waliohudhuria-
1.
Edward Msaky – M/Kiti - LEKIDEA
2.
Joseph Shewiyo – Katibu -
3.
Martin M Kessy
4.
Paul Msaki
5.
Thomas Msaki
6.
Savinus Kessy
7.
Venance V Msaki
-------------------------------------- --------------------------------------
Katibu M/Kiti
LEKIDEA
---------------------------------------------------------------------
ZIFUATAZO NI BAADHI TU YA PICHA ZA MATUKIO YA UJENZI KATIKA MAENEO MBALIMBALI YA BARABARA ZETU ZA LEGHO-KIRUA VUNJO MASHARIKI, MRADI UNAOSIMAMIWA NA TAASISI YETU YA LEKIDEA.
---------------------------------------------------------------------
KAZI ZAIDI ZINAENDELEA, UWEKAJI NA USAMBAZAJI WA MORAM KATIKA NJIA ZOTE MUHIMU, IKIWA NI PAMOJA NA KUKARABATI MAENEO KOROFI ENDAPO MVUA ZITALETA HITILAFU YOYOTE, HAYA YOTE TATAFANYIKA VYEMA.
KADHALIKA, NJIA ZA VITONGOJI PIA ZIMEPEWA KIPAUMBELE HASA KWA MICHANGO YA WAZALIWA WA MAENEO HUSIKA (AU FAMILIA) AMBAPO NJIA HIZO ZINAPITA. WANAWEZA KUJIUNGA NA KUCHANGIA KWA PAMOJA KUIMARISHA MAENEO YAO. WACHANGIAJI WANAWEZA KUCHANGA NA KUELEKEZA KUWA 'MCHANGO WANGU/WETU WA GREDA/MORAM AWAMU HII UKAFANYIE KAZI KATIKA NJIA AU MTAA/KITONGOJINI KWETU'...LEKIDEA IPO TAYARI NA ITAJITAHIDI KUTIMIZA HILO KULINGANA NA UMOJA WA WAHUSIKA NA HALI HALISI NA KIWANGO CHA WACHANGIAJI HAO ILI KUTOKUSABABISHA TATIZO.
TUCHANGAMKE, MUDA NDIO SASA, KUJENGA ASILI YETU.
TUCHANGAMKE, MUDA NDIO SASA, KUJENGA ASILI YETU.
PAMOJA TUTAFIKA NA KUFANIKIWA. TUUNGANISHE NGUVU!
TUCHANGIE BILA KUKATA TAMAA, NI MAENDELEO YETU WENYEWE.
---------------------
Michango ya LEKIDEA inaweza kuwasilishwa kwa CASH au kwa njia zifuatazo.
CRDB A/C: 0152095786500;
LEGHO KIRUA DEVELOPMENT ASSOCIATION
Kwa Simu: Vodacom MPESA– 0755 799 133; TigoPESA- 0653 799 133
Kwa Simu: Vodacom MPESA– 0755 799 133; TigoPESA- 0653 799 133
Muda ndio sasa, TUCHANGIE, TUENDELEE MBELE!!.
TYK...
Secretariat - LEKIDEA
No comments:
Post a Comment