LEKIDEA FOCUS OVERVIEW

LEKIDEA
is a registered Non-profit Organization of Kirua Vunjo East Moshi, by Natives from related Villages (Kileuo, Mrumeni, Kotule, Mero, Legho, Lasso, Kwa-Laria(Kanji), dedicated to join together, leverage their Vision, Objectives, Social strengths, ambitions & professionalism and other common resources from members, relatives and families having any origination with K.V East, to come TOGETHER, DEVELOP and CHANGE their Motherland through Projects and involvements in different Social development Initiatives that play roles in alleviating poverty and enhancing opportunities in collaboration with all well wishers, and support from social development entities from the village level, national level, and international level.

LEKIDEA :: Suala la Elimu na Ufundi

LEKIDEA IMEPANGA MIKAKATI MBALIMBALI KATIKA KUKUZA NA KUHAMASISHA ELIMU BORA NA SIO 'BORA ELIMU'. HIVYO NI DHAMIRA KUBWA YA LEKIDEA KUFUATILIA MASUALA YOTE YA UWEPO WA ELIMU BORA KATIKA UKANDA WETU WOTE KUANZIA NGAZI YA AWALI, SHULE YA MSINGI, SEKONDARI, UFUNDI NA HAYA HATUA ZA UANZISHWAJI WA VYUO KATIKA UKANDA WETU. VIJANA WETU WENGI WAO WANAO UWEZO MKUBWA LAKINI KUTOKANA NA KUKOSA NAFASI, MARA WAMALIZAPO MASOMO YA MSINGI AU SEKONDARI HUKIMBILIA MIJINI NA KUFANYA VIBARUA AMBAVYO NI NADRA SANA KUWAPATIA UFUMBUZI NA MAFANIKIO YA MAISHA YAO YA BAADAYE. 

ELIMU BORA KWA NGAZI ZOTE NDIO MSIMAMO, DHAMIRA NA MSISITIZO WA LEKIDEA SASA NASIKU ZOTE.

Huu sio wakati wa Watoto wetu kule Vijijini kusoma elimu ya Awali au ya Msingi katika Mazingira kama haya. Ni Hatari sana, na hili liepukwe kwa nguvu zote, na huu ndio msimamo wa LEKIDEA.


Ili Watoto wetu wasitawi Vyema Kielimu, LEKIDEA imeweka kipaombele kabisa kuwezesha Elimu katika mazingira kama yanavyoonekana kwa watoto hawa kuwa jambo muhimu Vijijini kwa Shule za awali na msingi.
Shule yao ya Msingi ikiwa njema na Vifaa vya Kutosha, inajenga uelewa wa Wanafunzi na hivyo kuwa na msingi bora kuelea Elimu ya Sekondari.

Elimu ua Sekondari pia inapokuwa bora, huwapa watoto wetu uhakika wa kuvuka vyema na kuingia Ngazi ya Vyuo

Sekondari Bora ni Hatua bora kuelekeo Vyuo mbalimbali, hivyo watoto wetu yafaa kuendelezwa kwa misingi hiyo wapate kuhitumu vyema.

LEKIDEA inatambua kuwa, Elimu Bora Hujulikana kwa Matokeo yake na pia jinsi inavyojali maendeleo ya watoto kiafya na kimazingira, na hatimaye ufaulu wa uhakika. Shule Bora za Sekondari kama hii, ndio Malengo Mifano Bora ndio Malengo ya LEKIDEA siku zote.



Hatimaye Vyuoni Mafanikio huwa yakinifu na Hivyo kuzidi kujenga kizazi chenye wananchi wenye ufahamu, uwezo na kunufaisha jamii walikotoka na pia Taifa kwa Ujumla wanapotumikia katika nyadhifa na Majukumu mbalimbali ya kijamii, ikiwa ni pamoja na Biashara kwa Umakini na Uangalifu ili kulinda kipato na faida.
SIASA HUVURUGA MAENDELEO YA ELIMU, TUEPUKANE NA MAENEO YA KISIASA YASIYOJENGA UTEKELEZAJI WA MALENGO YETU YA ELIMU KWA UKANDA WETU. LEKIDEA HAINA SIASA, HAIFUATI CHAMA CHOCHOTE CHA SIASA, BALI INASHIRIKIANA NA CHAMA CHOCHOTE KINACHOLENGWA KUENDELEZA JAMII YETU KATIKA NYANJA ZOTE.

3 comments:

Anonymous said...

Tumefurahi kuona blog na itasaidia sana kumaliza changamoto zinazotukabili wana lekidea

beda

Paul Msaki said...

Shukrani sana ndg, haya yote ni mema na yanawezekana kwa umoja wetu. Tupo pamoja, tutafika.

Anonymous said...

Kirua Vunjo Mashariki tunasonga mbele, nia tunayo, uwezo tunao, sababu tunayo!!