MRADI MKUU WA BARABARA YETU;
LEKIDEA IMEWEKA KIPAOMBELE KIKUU KATIKA UKARABATI WA BARABARA YETU KUU YA KUANZIA UCHIRA - KARUMELI HADI JUU KWA-LARIA (KANJI), NA MRADI HUU UNAJUMUISHA PIA BARABARA NDOGO ZINAZOTOKA VIJIJINI NA VITONGOJI VYOTE MUHIMU IFUATAVYO, KISOMACHI - HADI LEGHO (KNCU) KUPITIA KISANJA, KISOMACHI HADI KWA-RENE
(SUMI) KUPITIA KNCU, KNCU HADI KILASANIONI KUPITIA USANGI, KITAARINI HADI LASSO-KIWELEWELE KUPITIA KWA-MATAY,
MANZAONI, KAMA BAADHI YAKE ZINAVYOONYESHWA KATIKA RAMANI ILIYO CHINI.
MRADI HUU WA UKARABATI WA BARABARA ZETU NI SEHEMU YA MIRADI MINGINEYO MINGI AMBAYO LEKIDEA KAMA TAASISI YETU RASMI IMEIWEKA MEZANI TAYARI KWA AJILI YA UHAMASISHAJI NA MIKAKATI YA UTEKELEZAJI WA HARAKA NA WA UFANISI.
RAMANI HII INAONYESHA PICHA YA JUMLA YA MRADI WENYEWE NA UPANA WAKE, AMBAPO NGUVU, JUHUDI NA USHIRIKIANO WA KILA MWANA-KIRUA VUNJO MASHARIKI, TAASISI NA IDARA ZA KUJAMII NA KISERIKALI ZA KIKANDA ZITAHUSISHWA.
Kama ilivyoonyeshwa katika Ramani juu, Mradi huu ndio muhimu sana kwa Ufanisi, kuondoa Umaskini na udhaifu wa Jamii yetu yote inayotegemea sana Barabara ya Uchira hadi Karumeli hadi Kwa-Laria (Kanji). Pia Mradi huu utajumuisha Njia zitokazo katika Vijiji na Vitongoji Muhimu vya Ukanda wetu, ikiwa ni pamoja na Legho, Lasso, Kwa-Laria, Mero, Usangi, Manzaoni, Kileuo, Kotule, Mrumeni na Kileuo Kati.
LEKIDEA imeweka Mikakati ya Kuhusisha wanajamii wa Kada zote katika shughuli nzima za Ukarabati na Usafishaji wa Njia na Barabara hizi, ikiwa ni pamoja na Wananchi wa Vijiji tajwa kuandaa Siku rasmi za Nguvu-Kazi au Harambee (ilijulikana awali kama 'Jumatatu'), na hii itajumuisha Uongozi kwa ngazi za Mitaa, Vijiji na Kata, na pia Wenyeviti wa Kada zote hizo pamoja na Diwani wetu Mh. Alex Umbella; watakuwa ndio Mihimili mikuu ya Usimamiaji kazi na utekelezaji.
Kadhalika LEKIDEA imeweka lengo kushirikisha Taasisi zote za Kijamii ikiwa ni pamoja na Makanisa wa Makanisa yote, Karumeli na Legho, na pia mengineyo madogo-madogo, katika kuhamasisha Wanajamii wote walio katika Ukanda wetu kujituma, kuwajibika na kuendeleza juhudi la LEKIDEA za ukombozi wa eneo letu.
LEKIDEA imekusudia kuwa Mstari wa mbele katika Kushirikiana na Halmashauri na Kamati Tendaji, na pia Mfuko wa Jimbo la Vunjo, unaosimamiwa na Mbunge wetu, Mh. Augustine Lyatonga Mrema, ili kuhakikisha kuwa kila senti iliyotengwa kwa ajili ya maendeleo ya Ukanda wetu inapatikana, na inasimamiwa vyema ipasavyo katika kukamilisha miradi yetu yote, tukianzia na huu mradi mkuu wa Barabara zetu.
JAMBO LA MUHIMU NI UHAMASISHAJI, TUUNGANE WOTE, TUSHIRIKIANE WOTE, TUCHANGIE MENDELEO HAYA ILI TUJIKOMBOE, TUONDOKANE NA AIBU YA MIAKA YOTE YA 'KUWA NYUMA' KULINGANA NA KANDA NYINGINE ZA MKOA WA KILIMANJARO, MKOA ULIOPEWA NEEMA NA KUJULIKANA DUNIA NZIMA, BALI SISI TUNAJIDHARAU NA KUSAHAU UMUHIMU WETU NA ENEO LETU.
TUKIANZA VYEMA, TUKIHAMASHISHANA WOTE NA KUENDELEA MBELE, WENGINE WATAIGA NA WATATUUNGA MKONO. TUSHIRIKIANE KATIKA MRADI HUU WA BARABARA ZETU, NA HESHIMA ILIYOPOTEA ITARUDI MUDA SI MREFU:
LENGO KUU NA MUHIMU, TUSHIRIKIANE, TUUNGANE NA TUCHANGIE MAENDELEO HAYA MUHIMU KWETU NA KWA VIZAZI VIJAVYO NA TUNAYOYAFANYA LEO YATAKUWA KUMBUKUMBU KUU NA HISTORIA YETU NA VIZAZI VYETU VYOTE.
______________&&&&___________
MIRADI MINGINEYO
LEKIDEA IMEWEKA PIA MIKAKATI KAMILI KATIKA MIRADI MINGINEYO MBALIMBALI KWA AJILI YA JAMII NZIMA IKIWEPO MAENDELEO YA VIJANA NA WANAWAKE NA HARAKATI ZA UHAMASISHAJI NA USHIRIKIANO IKIJUISHA TAASISI MUHIMU ZA KIJAMII NA ZA KISERIKALI IPO MEZANI KWA AJILI YA UTEKELEZAJI MAPEMA IWEZEKANAVYO, HASA MARA YA BAADA YA MRADI HUU MUHIMU WA BARABARA KUSONGA MBELE, MAANA NDIO UTAKAOFUNGUA NJIA NA NAFASI KWA WANANCHI WETU KUFAIDI MAENDELEO NA BIASHARA ZA NDANI NA NJE YA UKANDA WETU.
MIRADI MINGINE IMEAINISHWA KATIKA MTIZAMO WA PICHA NA MAELEZO KATIKA KURASA ZILIZOPO KATIKA MTANDAO HUU WA LEKIDEA. WOTE TUNAOMBWA KUPITIA KURASA HIZO KWA UTULIVU NA KUCHAMBUA MIRADI ILIYOAINISHWA, ILI KUTOA USHAURI, MAPENDEKEZO NA MIKAKATI ZAIDI YA KIUTEKELEZAJI, NA YOTE HAYO YATAPOKELEWA NA KUFANYIWA KAZI LA UONGOZI WA LEKIDEA.
________________&&&&_______________
TUPO PAMOJA, TUSHIRIKIANE, TUTAFIKA HARAKA!
--________________&&&&_______________
--
--________________&&&&_______________
--