KATIKA UKURASA HUU MAMBO MUHIMU YATAHUSISWA:
MAKALA NA TAARIFA MBALIMBALI KUTOKA KATIKA JAMII YETU NA KWINGINEKO TANZANIA KATIKA KUKUZA UFAHAMU NA UKUAJI WA MAENDELEO YA KIJAMII ITAKUWA INATOLEWA HAPA: HASA KUJIHUSISHA NA KUSHIRIKIANA NA
- TAASISI MBALIMBALI ZA KIMAENDELEO ZA KITAIFA.
- TAASISI MBALIMBALI ZA KIMAENDELEO ZA KIMATAIFA
- USHAURI NA MAONI MBALIMBALI.
- NK.
-----------------------&&&------------------------
LEKIDEA KATIKA KUIMARISHA MASUALA YA AFYA NA USTAWI WA JAMII YETU VIJIJINI IMEKUSUDIA KUWEZESHA NA KUHAMASISHA HUDUMA MUHIMU ZA AFYA KWA WATOTO, WANAWAKE, WAZEE NA WALE NDUGU WASIOJIWEZA NA PIA WALEMAVU. HAYA YOTE YANAWEZEKANA KWA USHIRIKIANO NA TAASISI MUHIMU ZA KIMAENDELEO ZA KIKANDA, KIWILAYA NA HATA KITAIFA.
|
Huduma za Afya za namna hii haziwezi kulinda maendeleo ya wananchi wetu. |
|
Huduma Bora Vijijini, na Watoto wetu kulindwa zao hujenga Jamii imara. |
|
Walemavu na Wasiojiweza kiafya pia wanahitaji uangalizi wa Jamii yetu wote kuhakikisha wanajisikia kutambulika. |
|
Wazee na Wazazi wetu kama hawa Wanapata Amani na kushukuru pale tunapowapa Shukrani kwa kuwanasua katika hali ngumu ya kimaisha inayowakabili kwa sasa, jambo ambalo litathibitisha SHUKRANI YETU KWAO kwani ndio waliotulea na kutupatia Maisha ya sasa ya ustawi ambayo tunayaishi mijini, lakini tunawasahau, jambo ambalo ni makosa Makubwa. |
|
Zawadi pekee ya kumpa Mzee na Mzazi wetu kama huyu ni kumtunza kiafya, kimwili na Kimazingira, apate kufurahia uzao wake ambao ndio mimi na wewe, tunaoishi mijini na kuwasahau. Kitochi au Albam moja kumpa mzazi kama huyi amani ya kweli na kujua hakika amezaa kwa manufaa anapojumuika na wengine baada ya kazi zake. |
|
Kitokana na Majukumu ambayo wameyatekeleza kwa miaka mingi kama Wazazi wetu, ikiwa ni pamoja na kujinyima na kutupeleka shule, kukesha mashambani ili wapate kiasi kidogo cha fedha kulipia afya, ada, na mahitaji mengine ya familia zetu vijijini, Wazee hawa, ambao ndio wazazi wetu asili, wanahitaji kujengewa uhakika wa kujikimu wawapo katika mapumziko baada ya kazi zao, ikiwa ni pamoja na kupata kinywaji kigogo 'Mbege - Kitochi' ili wapate amani na kufahia uzao wao. Tuwajali, tuwafikirie, tuendeleze Barabara za Nyumbani kwetu ili Wazazi hawa wapate kufikiwa na kusaidiwa kirahisi. |
No comments:
Post a Comment