TAASISI NA WADAU MUHIMU KATIKA MALENGO NA MAJUKUMU YA LEKIDEA:
HALMASHAURI YA KATA YA KIRUA VUNJO MASHARIKI
Katika kuhakikisha kuwa Taasisi yetu ya LEKIDEA inaendesha na kukamilisha vyema majukumu yake, kutumikia wananchi wa Ukanda wote wa Kirua Vunjo Mashariki, Vijiji na Vitongoji vyake, LEKIDEA imeweka Malengo, na Utaratibu kamilifu katika kuhusisha Taasisi na Wadau muhimu wa maendeleo hasa katika ngazi ya Kata Yetu tukimshirikisha kwa ukaribu kabisa Diwani wetu makini Mh Alex Joseph Umbella
Mh. Alex Joseph Umbella
|
Diwani wetu Mh Umbella, (pichani juu) mara zote amekuwa akifanya kila juhudi kushirikiana na Halmashauri na Kamati Tendaji ili kuhakikisha kuwa fungu na haki ya Wananchi wote wa Kirua Vunjo Mashariki vinasimamiwa bila kutetereka. Wote tumuunge mkono, tuungane na wananchi wa Kata yetu hii na kuhakikisha kuwa malengo na majukumu yaliyo mbele yetu, yanayosimamiwa na LEKIDEA yanakamilika, na maendeleo tunayaona.
----------------------&&&&----------------------
OFISI YA MBUNGE - JIMBO LETU LA VUNJO
Kadhalika, juhudi kubwa zinazofanywa na Ofisi ya Ubunge - Jimbo letu la Vunjo ni juhudi ambazo zinafaa kuwekwa mstari wa mbele katika Kujenga na kuimarisha maendeleo ya Ukanda wetu katika miradi yake mbalimbali, na hasa Mradi mkuu wa Barabara ya Uchira - Karumeli hadi Kwa-Laria, ambayo hata Mbunge wetu Mh Augustine Lyatonga Mrema bila shaka, analifahamu tatizo kuu hili la barabara zetun toka wakati wa kampeni, na pia, kwa kutambua ufuatiliaje wake na umakini wake katika idara nyingi (Mfano Ufuatiliaji wake katika Kamati ya Bunge - Hesabu za Halmashauri).
Mh Augustine Lyatonga Mrema (MB) |
Mheshimiwa Mrema, Mbunge wa Jamhuri ya Muungano kupitia Jimbo laVunjo, (pichani juu) amekuwa mfuatiliaji mahiri wa masuala ya maendeleo na haki za wananchi wa ngazi zote. Tukikumbuka suala la Ulinzi na Usalama wa Ukanda wetu, Mh. Mrema mbali na kuweka kipaombele katika Barabara yetu, pia anayo nafasi kuwa kuwezesha kujengwa kwa Kituo Kidogo cha Polisi - pale Karumeli - Madukani. |
Mh Mrema, ameonyesha dhamira kamili ya kuunga mkono juhudi za LEKIDEA, na hadi sasa ametoa ahadi kuchangia kiasi cha Sh 2,000,000/ (Milioni mbili) kuunga mkono Maendeleo yatu yanayopiganiwa na LEKIDEA.
Tupo pamoja naye na kwa kuwa ufuatiliaji wake unaofahamika kwa miaka yote, bila shaka atakuwa bega-kwa-bega zaidi na jamii yetu ya KV-Mashariki katika kusonga mbele na kufikia tunakokusudia.
----------------------&&&&----------------------
No comments:
Post a Comment