LEKIDEA :: MAJI NA SALAMA
LEKIDEA MBALI NA KUTAMBIUA UMUHIMU WA AFYA YA JAMII YETU, PIA IMEWEKA KIPAOMBELE KATIKA KUHAKIKISHA KUWA MAJI YA UHAKIKA, SAFI NA SALAMA YANAPATIKANA KWA WANAVIJIJI WA UKANDA WETU WA KIRUA VUNJO MASHARIKI.
MAISHA YA WANANCHI YANAWEZA KURUDI NYUMA SANA, AU KUCHELEWA KUSONGA MBELE KUTOKANA NA MUDA MWINGI KUTUMIWA NA WANAVIJIJI KUHANGAIKIA MAJI, NA KUACHA KUFANYA KAZI ZA KUJIKWAMUA, AU KUZITUNZA VYEMA FAMILIA ZAO. PIA KWA KUKOSA MAJI SAFI NA SALAMA, UHAKIKA WA WANANCHI KUISHI BILA MAGONJWA UNAONDOKA, NA HIVYO WENGI HUUGUA MAGONJWA YA KUAMBUKIZA AU YA TUMBO YANAYOTOKANA NA WADUDU KWA KUNYWA AU KUTUMIA MAJI YASIYO SAFI NA SALAMA. LEKIDEA IMEKUSUDIA KUWAONDOLEA WANANCHI MATATIZO YOTE YATOKANAYO NA SHIDA YA MAJI, AU MATUMIZI YA MAJI YASIYO SALAMA.
|
Maji ni Uhai, Ila wananachi wanapokosa maji safi na salama, hutumia maji ambayo matokeo yake huindoa hata uhai uliokusudiwa, kama inavyoonekana mwananchi picha juu bila ku |
|
Katika hali kama hii, je maisha ya usalama na afya yanapatikana? Ni vigumu sana kulifikiria hilo, ila LEKIDEA ipo tayari kuhakikisha kuwa wananchi wetu wanaondokana na hali kama hii popote pale vivivini katika ukanda wetu. |
|
Watoto wetu ni hazina yetu ya baadaye, na wanastahili kulindwa na kuhakikisha kuwa shida za kijamii haziwakwamishi kupata elimu na kukua katika makuzi sahihi. Katika kuhakikisha kuwa watoto wetu wanapata elimu bora, huduma ya maji ni sehemu ya mafanikio ambayo yanawafanya watoto watulie mashuleni badala ya kuhangaika kama inavyoonekana juu, LEKIDEA inalitambua hili na imeweka vipaombele kuhakikisha maji yanapatikana kwa jamii nzima. |
|
Shida ya maji inaondoa amani na utulivi, kama anavyoonekana mtoto huyu. Jamii yetu haistahili kukumbana na hali kama hii. LEKIDEA imefanya juhudi kuliondoa tatizo hili kwa jamii yetu. |
|
Matatizo kama haya yanatoa sura kuwa siku zote wananvhi watakuwa wanahangaika katika kutafuta maji ambayo sio safi na salama, kama inavyoonekana juu. |
|
Katika hali kama hii, mama huyu atahudumia familia, au kufanya kazi za maendeleo? Na poa Mtoto aliyembeba anakumbana na hali ya maisha magumu, na shida za kijamii hata kabla ya kufikia muda na umri wake. |
|
Kutafuta Maji katika mazingira kama haya, ni hatari sana kwa uhai na usalama wa Mama na Mtoto. Katika mazingira kama haya, mama na mtoto wapo katika hatari ya afya na pia kuumia kutokana na miamba iliyo juu yao katika pango wanalochojoa maji. LEKIDEA itahakikisha kuwa wanaviji wetu hawakabiliwi na hali kama hii. |
|
Huduma ya maji inapokosekana, hata mifugo yetu inatupa picha ya shida iliyopo katika jamii. Hapa Bata wanaonekana wakihangaikia maji katika bomba hii, lakini bahati mbaya hayatoki. |
|
|
Haya ni Masikitiko na kukosa matumaini, kama anavyoonekana mtoto huyu akiwa katika kuhangaikia kupata maji, bila shaka yupo pamoja na wazazi wake. Katika umri wake huu, atavimilia na kujenga maisha gani na kuchangia maendeleo? |
|
Ukosefu wa maji hufanya wanawake na watoto wengi kuhangaikasiku nzima kuhangaikia maji na siku nzima kuweza kupotelea katika kuhangaikia maji kama inavyoonekana pichani juu. |
|
Wananchi wa Ukanda wetu wakishirikishwa vyema kuandaa miradi ya maji, watashiriki katika uchimbaji mitaro ya kulaza bomba za maji safi kama inavyoonekana juu. |
|
Kadhalika, katika kukuza maji na miradi mikubwa ya maji, kama umwagiliaji, na wananchi wanafarijika sana na kuhamasika, kuchimba mitaro mikubwa ya maji kwa matumizi ya kawaida na umwagiliaji kama inavyoonekana juu. |
|
Pale Mradi wa maji unapokamilika, wananchi huwa na raha na amani, kama inavyoonekana juu, wanafunzi wakifurahia uzinduzi wa maji. LEKIDEA imeyaweka malengo yake kamili kuhakikisha wananchi wetu wanajenga furaha ya kweli kwa kupata huduma ya maji. |
|
Maji safi na salam ya uhakika yanajenga amani na utulivu, hivyo kama inavyoonekana juu mwanafunzi akifurahia kuchota maji karibu kabisa na shuleni. Je kama maji yasingekuwa jirani na shule mwanafunzi huyu angewezaje kufurahia maji kama anavyoonekana mtoto huyu! LEKIDEA inakusudia kuhakikisha kuwa maendeleo yetu hasa kuhusu suala la Maji safi, linawagusa kila mtu kuanzia watu wazima hadi wanafunzi. |
|
Amani na Utulivu anaouonyesha mama huyu katika kicheko chake ni ishara kuwa ili maendeleo yapatikane, amani na utulivu, hasa pale huduma sahihi hasa kuhusu maji safi na salama yanapopatikana kwa uhakika kama inavyoonekana juu. LEKIDEA inalenga kujenga furaha kama hii kwa wazazi wetu, akina mama na watoto wa vijiji vya ukanda wetu. |
|
Katuni hii inatupa picha na jibu la miaka mingi kwa kilio chetu na cha jamii nzima kuwa, maendeleo kama ya maji ni wimbo wa kila siku ila bila ya juhudi kamili, tutabaki tunahangaika na kushindwa kufanya mambo ya maendeleo. LEKIDEA imejipanga kuhakikisha kuwa maji ni sehemu ya maisha na mafanikio ya kila siku ya mwananchi wetu. (Katuni kwa hisani ya Masoud Kipanya) |
LEKIDEA TUPO PAMOJA, TUNASONGA MBELE....MAJI NI UHAI..PAMOJA TUTAWEZA!
No comments:
Post a Comment