KAMPENI MPYA!!..."SAMBAZA KIKOMBE CHA UPENDO... JAZIA KOKOTO TUANZE KUWEKA LAMI UCHIRA - MAWONYI"
WAPENDWA WANA - KV NA WAZALIWA WOTE WA LEGHO KV MASHARIKI, ...AMANI NA UPENDO WA KRISTO NA VIWE KWA WOTE!!
NI UJASIRI WA PEKEE KWA KILA MWANA-LEGHO-KV TUNAPOPATA TAARIFA ZA MAFANIKIO TULIPOFIKIA SASA.
KWA UFUPI TU;-
* KUTOKANA NA TUKIO LA HARAMBEE YA PAMOJA YA "TOKOMEZA MAWE KWA LAMI" TULIWEZA KUKUSANYA KIASI CHA FEDHA NA KUTOA KARIBIA MILIONI 70 KUNUNUA MAPIPA 300 YA LAMI AMBAYO SASA YAPO TAYARI UCHIRA SEKONDARI KWA KAZI KUANZA.
* PAMOJA NA UFANISI WA KAZI HIYO KUBWA, WOTE KWA MOYO MMOJA TUMEENDELEA MBELE KWA UJASIRI NA KUANZA KAMPENI NYINGINE WAKATI WA KIPINDI KIFUPI CHA PASAKA "KUPANDA MBEGU KUPATA MIFUKO 200 YA CEMENT KUJENGEA MIFEREJI". KAMPENI HII NAYO ILIKUWA YA UFANISI MKUBWA AMBAPO KWA MIOYO YENU ILIYOJAA UPENDO, TULIWEZA KUKUSANYA ZAIDI YA CEMENT MIFUKO 500, YAANI UFANISI ZAIDI YA 250%.
* UKIJUMUISHA SALIO LA HARAMBEE YA " TOMOMEZA MAWE KWA LAMI" NA "KUPANDA MBEGU ZA PASAKA" TUMEKUTA TUMEKUSANYA ZAIDI YA MILIONI 55 [55,000,000/-] ZIPO TAYARI KTK AKIBA YA LEKIDEA. NI MAAJABU YA MUNGU, NA UPENDO HUU HAUNA MFANO NA KILA MZALIWA WA LEGHO-KV MASHARIKI ATAJIVUNIA UFANISI HUU NA ZAIDI NI PALE TUTAKAPOKAMILISHA LEGHO TUANZE KUTANDAZA LAMI!!
KWA KUJUA KUWA UPENDO WA KRISTO [ref MASOMO YA J2 YA ILIYOPITA] NDIO MSINGI NA UFANISI WETU, YAANI KUITOA NAFSI YAKO KAMA MWANA-KV, KWA AJILI YA MWENZAKO, AU JAMII YAKO, NDIYO MAANA KAMPENI HII MPYA INAFUNGUA UKURASA MUHIMU SANA KWA HATUA TULIYOKWISHAFIKIA SASA NA PALE TUNAPOELEKEA KUKAMILISHA HIVI KARIBUNI.
* KULINGANA NA MAKADIRIO GHARAMA ILIVYOANDALIWA KWA UMAKINI NA MAENGENEERS WA LEKIDEA [DSM NA MOSHI]; JUMLA YA KIASI CHA MILIONI 123 KILIKUWA KINAHITAJIKA KUFANIKISHA UWEKAJI WA LAMI 2km, KUANZIA UCHIRA HADI JUU YA MAWONYI [kwa Lotoronge], SEHEMU AMBAYO ITAWEKA HISTORIA YETU JUU!
TUKIZINGATIA KUWA TAYARI 'AKIBA' YA LEKIDEA SASA INAYO MILIONI 55 TAYARI...TUNATAKIWA ANGALAU MILIONI 35 HADI 45 KAZI IPATE KUANZA MARA MOJA MWISHO WA MWEZI HUU WA 5 MVUA ZITAKAPOISHA.
MATERIALS YANAYOHITAJIKA KUANZA UJENZI:
* KULINGANA NA VIFAA [MATERIALS] WALIVYOAINISHA VYEMA MAENGINEERS WETU, VIFAA MUHIMU SANA NI PAMOJA NA KOKOTO ZA KIA [AGGREGATES], PAMOJA NA CHANGARAWE [MORRUM] ZA MABUNGO AU PUMWANI. MATERIALS HAYA NDIYO YANATANDAZWA NA KUSHINDILIWA IMARA ILI KUJENGA MSINGI [BASE] KABLA YA KUMWAGA LAMI. MATERIALS HAYA AINA MBILI [AGGREGATE (trip 46) NA MORRUM (trip 400)], JUMLA YAKE INAFIKIA SH 35,000,000/- [MILIONI 35]. HIKI NI KIASI AMBACHO KINAWEZA KUPATIKANA HARAKA TOKA KTK AHADI ZA ZAMANI NA WALE WAPYA NA PIA KWA WALE WALIOKWISHAMALIZA AHADI LAKINI KWA UPENDO WAO WANAWEZA KUENDELEA KUJAZIA KTK "KAMPENI YA KUJAZIA KIKOMBE CHA UPENDO - KOKOTO NA MORRUM TUWEKE LAMI".
* KWA MCHANGANUO HUO NA UFANISI TULIOFIKIA SASA KAMA 'WAZALIWA WA MAMA MMOJA - MAMA KV' YUNAWEZA KUKAMILISHA KWA KUSHIRIKISHANA KUCHANGIA KIDOGO HADI KIKUBWA KAMA TUNAVYOJALIWA.
* NDIO MAANA KILINGANA NA MASOMO YA IBADA YA JUMAPILI ILIYOPITA, UPENDO WA YESU NDIYO UJUMBE KAMILI, NA NI MUHIMU SANA KWETU...TUUNGANE PAMOJA KUIZINDUA KAMPENI YETU MPYA...
KAMPENI MPYA YA..."SAMBAZA KIKOMBE CHA UPENDO... JAZIA KOKOTO TUANZE KUWEKA LAMI UCHIRA - MAWONYI",
KAMPENI HII NI YA MWEZI MMOJA TU, ITAKAYOTUPA NEEMA MPYA KUHAKIKISHA TUNAKUSANYA HIYO MILIONI 35 AU ZAIDI, NA MARA IFIKAPO TAREHE 10 MWEZI WA 6, TUTAWEZA KUWA NA MILIONI 90 AU ZAIDI, NA AWAMU HII ITAFUNGWA RASMI ILI KAZI IANZE UCHIRA.
TUNAWEZA! TULIWEZA KUCHANGIA (2009 - 2012) KUJENGA KANISA [ZAIDI YA MILIONI 500], TULIWEZA KUCHONGA NJIA ZA VIJIJI VYA KATA YETU (2012-2013) NA KUWEKA MORRUM 18KM [ZAIDI YA MILIONI 96], TULIWEZA (2014 HADI SASA) KUCHANGIA NYUMBA YA MAPADRE [ZAIDI YA MILIONI 55]. JE TUTASHINDWA HII MILIONI 35 HADI MILIONI 45?...TUNAWEZA! TUPO IMARA!
MOTTO WETU;-
KAMPENI MPYA!!..."SAMBAZA KIKOMBE CHA UPENDO... JAZIA KOKOTO TUANZE KUWEKA LAMI UCHIRA - MAWONYI"
Tunamwomba kila MMOJA wetu awe Nabii kwa kila mwana-KV mwenzake, amsambazie KIKOMBE CHA UPENDO na KUHAKIKISHA KILA M-KV KTK KANDA ZOTE TANZANIA, anajumuika tuwe pamoja KUCHANGIA ndani ya huu MWEZI MMOJA pekee.
Ujumbe huu utawekwa ktk UKURASA wetu wa Facebook na ktk mtandao wetu wa www.LEKIDEA.blogspot.com.
TUKISAMBAZE KIKOMBE CHA UPENDO..!!
PICHA ZA MATERIALS ZITAAMBATISHWA SOON!
MICHANGO ni KUPITIA AKAUNTI ZA LEKIDEA-MPESA - 0765 189 122 (Paul Msaki) na CRDB BANK Na 0152095786500 (Legho Kirua Dev Assoc.)
"PAMOJA DAIMA, TUTAFANIKIWA HARAKA ZAIDI"
WENU;
Sekretariat - LEKIDEA.
10/05/2015
AGGREGATE (KOKOTO ZA KIA) zinahitajika trips 46 |
MORRUM WA MABUNGO AU PUMWANI, unahitajika trips 400. |
No comments:
Post a Comment