Wana-LEKIDEA,
Lifuatalo ni Tangazo la Tender ya Ujenzi wa Barabara yetu ya Uchira hadi Kisomachi, kama lilivyotolewa na Manispaa ya Halmashauri na kuchapishwa katika Gazeti la Mwananchi kama linavyoonyeshwa.
LEKIDEA KWA KUFUATILIA KWA UKARIBU MAENDELEO YOTE NA KUHAKIKISHA
KUWA MPANGO HUU UNATEKELEZWA KWA UWAZI NA KWA UIMARA ILI KUFANYA BARABARA YETU
IWE IMARA NA YA KUDUMU.
TUNAWAOMBA WANA-LEKIDEA WOTE WENYE
MAKAMPUNI YA UJENZI YALIKWISHASAJILIWA NA BODI YA USAJILI WA MAKANDARASI, WAWE
WA KWANZA KUTUMA MAOMBI YAO MAPEMA IWEZAKANAVYO, WAKIZINGATIA VIGEZO NA
MASHARTI YALIYOAINISHWA CHINI YA TANGAZO LENYEWE.
KATIKA TANGAZO HILO, MAMBO YAFUATAYO YAMEONEKANA KUTUGUSA NA PIA
YATAFUATILIWA KUJUA HASA UNDANI WAKE KATIKA UTEKELEZAJI PALE MKANDARASI
ATAKAPOPATIKANA:
- LOT
5
na LOT 8 kwa pamoja zimeainisha kuhusisha Ukarabati wa
Barabara yetu ya Uchira - Kisomachi - Jambo hili litafuatiliwa kuona kama
kuna double-allocation ya funds au vinginevyo ili kuhakikisha kila
kilichopangwa kinatumika vyema ipasavyo.
- LOT
6,
ina kipengele cha Ukarabati wa Barabara ya PAKULA hadi KILEMA. Katika
Mradi wa LEKIDEA kusimamia ukarabati wa Barabara za Vijiji na Vitongoji,
eneo la kuanzaia Kanji -kwa Laria hadi Lasso - Juu (Darajani), ni maeneo
ya Ukanda wa LEKIDEA pia. Hivyo uongozi wa Diwani wetu hakika utaombwa
kufuatilia ashirikiane na wanaohusika kusimamia kipande hiki kwani ni
muhimu sana katika kuunganisha wananchi wote wa Mero, Kwa-Laria
(Kanji), Lasso Kati na Lasso-Juu kwenda Kilema Sokoni (Lyamombi),
Marangu Mtoni na Soko la Mwika. Barabara hii ni rahisi sana kwa wananchi
hawa na ni fupi kwao pia. Hata usafiri utakuwa rahisi sana.
- Katika
Tangazo hilo, Ili kuwezesha Wana-LEKIDEA kufuatilia na kujionea yale
maeneo muhimu yanayotuhusu Ukanda wetu kwa ukaribu, nimezungushia rangi wa
chungwa/njano majedwali yanayohusika.
No comments:
Post a Comment