LEKIDEA imeweka mikakati kamili katika kuhakikisha suala la Ulinzi na Usalama katika jamii yetu yote ya Kirua Vunjo Mashariki inaimarika, inaaminika na inaleta utulivu wa uhakika kwa Wananchi wote na pia kwa wageni, ikiwa ni pamoja na kusaidia Shughuli na gharama za mafunzo ya Mgambo katika ngazi ya Vijiji na Malengo ni kufikia hata ngazi ya Kata nzima.
Mgambo Katika Mafunzo ya Ukakamavu |
Mgambo Wakiwa katika hatua ya mwisho ya Mafunzo tayari kwa Kazi ya Ulinzi |
____________________________&&&_____________________________
Kadhalika, LEKIDEA ina mtizamo wa kuhakikisha malengo ya Ujenzi wa Kituo kidogo cha Polisi katika maeneo ya Kati, na hususan maeneyo ya Karumeli - Madukani ili kuondokana na utegemezi wa Kituo cha Himo pekee ambacho mara nyingi mwananchi huchelewa sana kupata huduma sahihi na ya mara moja kulinda haki ya wananchi, pale inapohitajika haraka.
Kituo Kidogo cha Polisi kama hiki ni muhimu kwa eneo la Kata yetu ya Kirua Vunjo Mashariki |
Kituo kikiwepo, pia Askari wa doria watakuwepo kusaidia utulivu na Ulinzi kwa jamii nzima. |
TUSHIRIKIANE, TUFANIKISHE HAYA.
No comments:
Post a Comment