|
Msitu huanza kwa kupanda Mbegu kama hii...wote tushiriki kulinda na kupanda miti/misitu yetu. |
|
Hatimaye Vitalu ndio hufanya mkusanyiko wa miti mbalimbali inayofaa kutawanywa na kupandwa. |
|
|
Vitalu hivi vinahitaji kutunzwa kwa uangalifu na kuhakikisha kuwa miche inasitawi ipasavyo. |
|
Miche ikisambazwa na kuoteshwa vyema kufanya Msitu kukua na kubadili mazingira vyema. |
|
Hata pale Misitu imekuwa lakini ikadumaa, inabidi kuwajibika kwa kuendelea kupanda miche mipya. |
|
Msitu BORA
huleta Mvua, huimarisha kilimo, huongeza rutuba, na kufanya hali ya hewa
kuwa safi na kupunguza Ukame. Tuendeleze upandaji na kulinda misitu
yetu kwa kupanda Mbegu na miche ya miti ya kudumu...wote tushiriki
kulinda na kupanda miti/misitu yetu. |
|
|
Misitu inapokuwa bora, ardhi huwa bora na pia miundombinu, kama barabara huimarika na kuvutia katika hali halisi. |
MTIZAMO WA LEKIDEA:
LEKIDEA IMEKUSUDIA MENGI KATIKA UHIFADHI, NA UENDELEZAJI WA MALI ASILI NA MISITU KATIKA UKANDA WOTE WA KIRUA VUNJO MASHARIKI NA KIRUA VUNJO YOTE.
- MASUALA MBALIMBALI NA MALENGO YA LEKIDEA KATIKA KUSHUGHULIKIA NA KUHAMASISHA UHIFADHI NA USIMAMIZI WA MAZINGIRA IKIWA NI PAMOJA NA MALENGO YA UHAMASISHAJI UPANDAJI MITI, KUELIMISHA WANANCHI NA KUZUIA TABIA ZA UVUNAJI WA MITI NA UCHOMAJI WA MISITU.
- PIA KUSHIRIKIANA NA TAASISI NYINGINE NA MASHIRIKA MBALIMBALI YA KITAIFA, NA KIMATAIFA (NGOs) KATIKA KUHAKIKISHA UTUNZAJI WA MALI-ASILI NA MAZINGIRA NI WA HALI YA JUU NA NI KIPAOMBELE KWA JAMII NZIMA.
- KUSIMAMAIA MALENGO YETU KATIKA NGAZI YA MITAA, VIJIJI NA UKANDA WETU WOTE KWA KUHUSISHA WANANCHI, SERIKALI ZA MITAA, VIJIJI, KATA NA HALMASHAURI NA IKIWEZEKANA HADI NGAZI YA KIMKOA NA KITAIFA ILI KUHARAKISHA UTEKELEZAJI WAKE.