Ndugu
wana-LEKIDEA,
Tunawasalimu
wote tena kwa Jina la Mwenyezi na tunawapa pole kwa majukumu mengi ya mwaka
mpya.
Kama
mjiavyo, Sekretariet imekuwa inafanya kazi juu chini kuhakikisha kuwa jambo
muhimu tulilolianza linatekelezwa kama inavyotakiwa.
Awali
tulitegemea hatua za Halmashuri yetu lakini baada ya kuona kuwa zinachelewa
Sekretariat imeandaa 'mpango-kazi' wa utekelezaji kwa barabara zetu za, kule
juu kuanzia Kisomachi kwenda Vijijini. Wote tuelewe kuwa kwa kuwa hatuna
mamlaka ya kutengeneza barabara ya Uchira-Kisomachi bila kupitia
Halmashauri, ndiyo maana hatujaiweka katika mpango huu wa awamu hii ya sasa.
Halmashuri
itakapoanza ujenzi sisi bado tutaingia humo kama tulivyoahidi na kufafanua
katika mpango wa kwanza. Kwa sasa tunapendekeza utekelezaji uwe kwa LEKIDEA
kukubaliana na Mkandarasi wetu kuanza ujenzi wa barabara za vijiji zifuatazo
zenye jumla ya kilomita 12 (tazama barabara nyekundu
kwenye ramani iliyoambatanishwa chini).
BARABARA HUSIKA - AWAMU YA 1:
- Kisomachi
hadi Kwa-Laria kupitia Mero Kati- Kwa-Matay hadi Laso juu (Mkombenyi) kupitia Manzaoni-CCM na Kiwelewele
- Kisomachi hadi Kapero Center
- Kisomachi hadi Shule ya Kilimani kupitia Mrumeni
- Kitaarini hadi KNCU
Ndugu
wana LEKIDEA wote, kama mnavyoona kwenye jedwali la gharama tunaweza kuanza
ujenzi kwa hatua (1) (ktk Jedwali), ambayo ni kujenga mitaro ya maji na
culverts, Ili tuweze kuendelea na kuchonga barabara hizo (grading) namba
(2), kwa kiwango stahiki tutahitaji kubanana sana walikwishatoa pledge
tunawaomba wakamilishe na ambao bado wote tuungane watoe michango yao, na wote
tuhimizane kwa nguzu zote.
Nia
yetu ni kukamilisha hadi namba (3) ksms inavyoonyeshwa katika Jedwali,
ambayo ni Moram na compaction ni gharama kubwa lakini tunataka kila mtu ajitoe
hasa wale wengi ambao bado. Kadahalika tumewaomba wazazi waliopo katika Vijiji
vyote, wahimize watoto wao na wao wenyewe washiriki.
Tunatafuta
ushauri wa wataalamu kuhusu mvua za masika kama ni busara kuanza kabla au baada
ya mvua. Hata hivyo utekelezaji ni lazima, tumeanza lazima tufike. Sasa
tunaomba maoni yenu katika vipengele vyote ikiwa ni pamoja na namna ya kupata
fedha ya kutosha kukamilisha kazi hiyo muhimu katika hatua hii tunayotaka
kuchukua sasa.
Tunawategemea
sana Ngd Wafuatao katika kufuatilia na kutoa Mwongozo na Uangalizi katika mradi
huu muhimu: Eng Bernard D. Msacky, Eng. Simon Njau, Eng.Bona na
tunatangulia kuwashukuru WOTE kwa kufanya kazi hii endelevu na iweze kufanikiwa
vyema.
Tunawaomba
wote kutoa maoni na mawazo endelevu mapema NDANI YA WIKI MOJA, ili kufikia
muafaka ma kuwezesha mradi huu kuanza.
PAMOJA
DAIMA, TUTAFANIKIWA HARAKA.
TYK......,
SEKRETARIAT -
LEKIDEA,
------------------------------------------------------------------------------------------
RAMANI YA BARABARA HUSIKA KATIKA AWAMU HII:
MAKISIO YA GHARAMA KWA AWAMU HII YA 1
No comments:
Post a Comment