WANA-KV MASHARIKI (LEKIDEA)
SIKU YA JANA JUMAMOSI, ILIFUNGUA UKURASA MPYA. MWENYEKITI WETU NDG EDWARD FABIAN MSAKY ALIMKABIDHI RASMI OFISI KARANI WA LEKIDEA [STELLA NJAU] ILI KUANZA MAJUKUMU KESHO.
OFISI HIZO ZIPO GHOROFA YA 4, NDANI YA JENGO LA S & F HOUSE, JENGO LIPO MWANANYAMALA, [KOMA-KOMA], AMBALO KWA CHINI IPO BANKI YA AKIBA COMMERCIAL. JENGO HILO LINALOMILIKIWA NA MWANA-LEKIDEA, ENG. SIMON TEOBALD NJAU.
MUNGU AMEIJALIA SANA KV KUWA NA WATU WENYE MOYO WA KUJITOLEA, NA WENYE VIPAJI MBALIMBALI, NA WANABARIKIWA ZAIDI KWA JINSI WANAVYOJITOLEA.
ZIFUATAZO NI KATI PICHA ZA TUKIO HILO MUHIMU, PICHA ZINAANZIA NA JENGO LENYEWE, IKIFUATIWA NA MATUKIO A KUFUNGUA VIFAA NA KUUNGANISHA VIFAA HIVYO [COMPUTERS], KAZI ILIYOFANYWA NA KATIBU WA SECRETARIAT YA LEKIDEA [PAUL SANENE MSAKI].
PICHA NYINGINE ZATATUMWA PIA KTK MTANDAO Facebook, ktk KURASA WA LEKIDEA; Unatakiwa tu kutafuta [seach] Legho Kirua Development Association., utakutana na picha link ya picha hizo
TUFUATILIE, TUCHANGIE TUSONGE MBELE!!
PICHA NYINGINE ZATATUMWA PIA KTK MTANDAO Facebook, ktk KURASA WA LEKIDEA; Unatakiwa tu kutafuta [seach] Legho Kirua Development Association., utakutana na picha link ya picha hizo
TUFUATILIE, TUCHANGIE TUSONGE MBELE!!
PAMOJA TUSONGE MBELE!
PAUL MSAKI
Katibu wa Sekretariat - LEKIDEA.--------------------------------------------------------------------
Jengo la S & F likionekana kwa nje |
Mlango wa Kuingia ktk Ofisi za LEKIDEA, ghorofa ya 4 |
M/Kiti na Karani wa LEKIDEA wakiwa wamesimama pamoja na Vifaa ndani ya Ofisi ya LEKIDEA |
M/Kiti kimwelekeza Karani baadhi ya masuala ya Majukumu yake ikiwa ndio kukamilisha Makabidhiano kamili ya Offisi na Vifaa. |
Ofisi ya LEKIDEA inavyoonekana kwa nje! Ni Ofisi ya Kisasa kabisa yenye A/C [vipooza hewa] |
Katibu wa Secretariat ya LEKIDEA, ambaye pia ni Mtaalam wa Technolojia ya Mawasiliano [IT] akiunganisha Vifaa vya Ofisi tayari kwa kutumika. |
Katibu wa Secretariat akijaribu Computer baada ya kukamilisha ufungaji wake na hivyo kuwa tayari kwa Karani kuanza kazi rasmi. |
Karani wa LEKIDEA Stella Njau akikalia usukani wa Ofisi yake tayari kwa kuanza kutekeleza kazi za maendeleo ya LEKIDEA |
WOTE TUUNGE MKONO, TUSHIRIKIANE TUFANIKISHE MAENDLEO YA UKANDA WOTE WA KIRUA VUNJO MASHARIKI IKIJUMUISHA MAENEO YOTE YA LEGHO, MULLO, LASSO, MERO, KILEUO, MRUMENI HADI UKANDA WA NGANJONI.
KARANI WA LEKIDEA ATAFANYA KAZI ZAKE KILA SIKU KUHAKIKISHA KUWA MAWASILIANO YANAWAFIKIA, NA MCHANGO WA KILA MMOJA WETU UNATAMBULIWA NA KUHESHIMIKA KATIKA KUCHANGIA MAENEO YA URITHI WETU PALE TULIPOZALIWA, YAANI KIRUA VUNJO MASHARIKI, INAYOSIMAMIWA NA TAASISI YETU RASMI YA Legho Kirua Development Association (LEKIDEA), iliyosajiliwa rasmi tangu 2008!
PAMOJA DAIMA TUTAFANIKIWA ZAIDI.
No comments:
Post a Comment