KIKAO CHA LEKIDEA;
Venue:–DOUBLE VIEW HOTEL
08/12/2011
MINUTES ZA KIKAO
|
||||||||||||||||||||||||
AGENDA
|
||||||||||||||||||||||||
1.
Kufungua kikao
2.
Chairman Statement
3.
HALI YA LEKIDEA kwa Kifupi – Status of
LEKIDEA
4.
Maendeleo ya LEGHO – KIRUA VUNJO
MASHARIKI (Makisio yaliotengwa na Halimashauri ya Wilaya ya Moshi (V)) –
Current Development and approved Budget For LEKIDEA areas.
5.
Taarifa Fupi ya Fedha Kuhusu Michango –
Bank Statement vs. Actual Contribution
6.
Mapendekezo Mapya Kuhusu Uchangiaji –
Additional Modality of Contributions
7.
The way Forward and End of the year
Strategies
8.
Kufunga Kikao
|
||||||||||||||||||||||||
MCHANGANUO
WA AGENDA
|
||||||||||||||||||||||||
1.
Kufungua kikao
Kikao kilifunguliwa kwa Sala saa 2.00usiku
na Katibu, Nd. Joseph. Shewiyo
2.
Taarifa ya Mwaka ya M/Kiti kwa
Wana-LEKIDEA (Chairman Statement).
·
Taarifa
ya M/Kiti iliwasilishwa na Makamu M/Kiti, Eng. Simon Njau kwa niaba ya
M/Kiti, ndipo baadhi ya Wajumbe kuchangia kwa maoni na hoja mbalimbali kama
ifuatavyo:
a. Ndg Emilian alipendekeza kuwa pamoja na
taarifa hiyo kuwasilishwa katika kikao hicho, itolewe pia kwa baadhi ya
wanachama waisome na wachangie kabla haijawasilishwa rasmi kwa jamii nzima ya
Wana-LEKIDEA. Wazo hili liliafikiwa, na taarifa hiyo iliwasilishwa kwa
wajumbe wafuatao:
i.
Prof. Ernest Mally – DUCE
ii.
Prof. Itika
- SUA
iii.
Prof.
Beda Kessy – SUA
iv.
Dr
. Valence Ndesendo – Wits Universiy- SA
Masuala
muhimu ya usimamizi wa majukumu ya sasa ya maenedeleo ya eneo letu yalijadiliwa
na hasa kwa kuzingatia Tangazo la Tender ya Ujenzi wa Barabara ya Uchira –
Kisomachi na pia barabara za vitongoji ambazo ni muhimu pia kwetu.
Awali,
Ufafanuzi wa Tender LOT 5 na LOT 8, ilivyoandikwa katika Gazeti la Mwananchi,
ulitolewa na Eng. Bernard Msacky, na pia Eng Simon Njau kama ifuatavyo:
·
LOT 5 – Kifungu hiki kilielezewa kuwa kazi
husika itajumuisha kurekebisha baadhi ya maeneo fulani Fulani kadri
itakavyohitajika na siyo ukarabati wa jumla wa barabara hiyo.
·
LOT 8 – Kifungu hiki kilielezewa kuwa
kinahusika na kazi ya ukarabati wa jumla wa barabara hiyo ambao kawaida unatakiwa kufanyika kila
mwaka.
Kikao
kilipendekeza katika kuhakukikisha hatua zote za awali zimapangika vyema na
hata pale kazi itakapoanza inasimamiwa ipasavyo, Diwani wetu Mh Alex Umbella
na baadhi ya Wahandisi wetu ambao wapo Moshi wahusishwe kwa Ukaribu sana.
Wahandisi hao ni Eng Bona Mathem, na Ndg Nevili Msacky.
Eng.
Simon Njau na Eng Dernard waliombwa waanzishe mawasiliano ya karibu na hao
Wahandisi waliopo maeneo ya kule kwetu ili waweze kusimamia kwa karibu suala
hili. Kadhalika ilipendekezwa kuwa, maongezi na Mhandisi wa Manispaa
yafanyike pamoja na Diwani wetu hasa wakati wa kuanza ujenzi.
·
Mjimbe
mmoja alipendekeza kuwa maeneo ya
vijijini ndizo muhimu zaidi na inatakiwa tujadiliane na Mkandarasi wa
Manispaa pamoja na Diwani ili kuangalia uwezekano wa kuhakikisha kazi
inafanywa hadi maeneo hayo, na iwe imara na ya kudumu.
·
Eng
Simon Njau aliahidi kuonana na Diwani ili kujua kama barabara iliyowekwa
katika Tender inayoonyesha kuwa Km 6.9 ni hadi Kwa-Laria au inaishia KNCU au
Kisomachi. Pia alipendekeza kuwa pale Mkandarasi atakapochanguliwa, kazi ya
kujenga maeneo ya vijijini yataunganishwa kama kazi ya ziada (additional
works) na gharama zake LEKIDEA itawajibika.
Malengo ya LEKIDEA katika Ujenzi huu:
Kuhakikisha kuwa pale Manispaa
itakapoishia, LEKIDEA itaendelea kukamilisha katika:
·
Maeneo
ya hiyo barabara kubwa ambayo yatahitaji uimarishwaji wa ziada kama mitaro ya
maji na culverts.
·
Barabara
za Vijijini na Vitongoji vyake kama zinavyoonekana kwenye ramani yetu.
·
Ilipendekeza
kuwa ni muhimu sana kuhakikisha kuwa maeneo muhimu tunayotoka yanakuwa
kipaombele, mfano Njia itokeayo Legho, ipitiayo Kisanja, Kwa Kikuyu hadi
Kisomachi, kwa mwaka mzima inakuwa inapita maji imeharibika na hakuna
suluhisho lililokwishapatikana la kudumu.
·
Ilipendekeza pia
kuwa matengenezo yatakayofanyika yawe ya uhakika na barabara ipitike kwa mwaka mzima –Diwani ahusishwe
·
Ni
muhimu Diwani awe ndiyo kiungo chetu na Halmashauri na pia katika kusimamia
makubaliano ya ziada kati ya Lekidea na Mkandarasi atakayeteuliwa na
Halmashauri
·
Kazi
ifanyike kwa uwazi na uhakika na LEKIDEA iwe inatoa taarifa hatua kwa
hatua maana uwazi ndio msingi wa
mafanikio.
·
Uongozi
wa Lekidea ufanye mazungumzo na Paroko na viongozi wa mitaa ili wananchi waweze
kutoa michango yao kwa mfano badala ya kusomba moram toka Kilindini upatikane
hapo Kisimajuu bure na pia nguvu kazi za wananchi katika matengenezo ya suku
hadi siku ya barabara hizo baada ya kutengenezwa.
·
Pia
kikao kilipendekeza kuwa baada ya barabara kutengenezwa, uwepo uwezekano wa
kupatikana gari katika kipindi fulani –lori hata la kukodi, litakalo kuwa
chini ya Diwani na Paroko ili kuendeleza kusimamia na kukarabati njia
(preventive maintenance) kwa nyakati mbalimbali.
4.
Taarifa Ya Fedha Kuhusu Michango – Bank
Statement vs. Actual Contribution
·
Kikao
kilipokea Taarifa ya Fedha kama ilivyowasilishwa na Ndg Emilian Saluo, ikijumuisha
Hali halisi katika benki na pia maendeleo ya ahadi kwa kila siku kama zinavyowasilishwa
kwa Sekretariat, na taarifa zote mbili ziliwiana kuhusu makusanyo
yalivyopokelewa benki hadi sasa. Ahadi zilikuwa zimefikia Sh. Milioni
49,816,000/- na Fedha Taslimu zilizokwishakusanywa ni kiasi cha Sh. 27,
616,000/- kwa hivyo kiasi ambacho bado wana-LEKIDEA waliohidi hakijawasili ni
Sh. 22,200,000/-
·
Kadhalika,
Kikao kilipokea kwa maendeleo na hamasa za michango inavyoenda, na taarifa za
Ahadi ya Ndg Paul Mremi Lyimo ya Sh 4,000,000/- (Milioni nne) ambazo
ataanza kulipa Milioni 2 ifikapo Tar 12/12/2011, na iliyobaki atawasilisha
Mkandarasi atakapokabidhiwa kazi na mara kazi ya ujenzi itakapoanza.
·
Kadhalika
Kikao kilipokea ahadi ya Dada yetu Lucy Alois Ndetiko Tesha ya Dola za Kimarekani 1,000/- (US$1,000)( ni karibia Tsh 1,600,000/-)
kama ilivyowasilishwa na Ndg Joseph Shewiyo, pamoja na ahadi nyingine kadhaa
toka kwa wana-LEKIDEA hadi sasa kama zinavyoendelea.
·
Pia
katika taarifa ya Ahadi, ilionekana kuwa kuna uwezekanao wa baadhi ya majina
ya watu wawili ambao ahadi zao hazikuweza kuifikia Sekretariat, na hivyo
ilipendekezwe waongezwe rasmi. Majina hayo ni:
§
Elinami Minja
- 1,000,000
§
Teye Anthony
- 1,000,000
5.
Mapendekezo Mapya Kuhusu Uchangiaji –
Additional Modality of Contributions
·
Mapendekezo Mapya ya Uchangiaji
Kuhusu idadi ya watu 56 ambao tayari
wameshatoa ahadi, kila mjumbe wa kikao alichukua listi yake ya watu ili
kugawana na kuwafuatilia wale ambao bado, au hawajakamilisha (Mgawanyiko huu umeambatishwa)
·
Kuongeza pledges zaidi:
Ilipendekezwa
kuwa ili list kuu ya sasa ya wana-LEKIDEA zaidi ya 400 itumwe kwa Emilian
Saluo ambaye ataweza kuchuja tena idadi ya watu wapatao 50 ambao
watawsilishwa ili wafuatiliwe kuchangia. Kikao kiliafiki hoja hii.
·
Pia
katika listi kuu, ilipendekezwa kuwa
majina zaidi yaongezwe katika
listi kuu ,watakao patikana 50 wafuatiliwe kwa simu, na hiyo ikikamilika
wengine pia wataandikwa na mzunguko
utaendelea hivyo. Kikao kiliafiki.
·
Pia
ilipendekezwa kuwa ili kuhamasisha zaidi kila mtu, kiwango cha nchini pia
kipendekezwe, mfano kuanzia 20,000/- hadi 50,000/- na pia 100,000/- hadi
200,000/- na kuendelea; hasa kwa ajili ya kuwahamasisha wanaosuasua, na watu
waelezwe haraka wachangie. Wazo hili liliafikiwa.
·
Pia
ilipendekezwa na kuwa kwa wale wanaomaliza kuchangia, tarifa fupi simu (SMS)
zitumwe kwa Wana-LEKIDEA wote ili taarifa ziwafikie pia wale ambao hawapati
email, na hili liliafikiwa.
·
Pia
itumike njia ya kuwatembelea watu katika maeneo mbalimbali ili kuwafikia wale
ambao hawajapata uhakika, au sio wepesi kuamua.
·
Kadhalika,
kikao kilipendekeza kwa sasa tutumie pia mfumo wa kuandaa Card zenye Jedwali,
kama zitumikazo makanisani kukusanya michango ya hiari, ili tuzitumie kuchangia/kukusanya
fedha hata kwa wale wasio wana LIKIDEA
kama marafiki na pia waheshimiwa viongozi, na zipatikane chache zenye mantiki
na zinazoonesha malengo kamili ya LEKIDEA. Hili liliafikiwa pia.
·
Card
rasmi ya michango kwa mtu mmoja mmoja iliwasilishwa na kupitiwa na wajumbe,
na marekebisho kidogo yalifanyika ambayo yataingizwa ipasavyo, na
zinatarajiwa kukamilika zichapwe mapema iwezekanavyo ili zisambazwe kabla ya
Christmas
6.
Utekelezaji na Mikakati iliyo mbele
yetu (The way Forward and End of the year Strategies) na Pia kuuanza Mwaka
Mpya
·
Mikakati
katika kukamilisha mwaka, majukumu
na mikakati kadhaa ikijumuisha malengo ambayo hayakuweza kukamilika mwaka
huu, na hivyo kuanza nayo kwa nguvu kubwa mwakani. Masuaka muhimu yaliyowekwa katika
utekelezaji kuelekea mwisho wa mwaka huu ni pamoja na kufuatilia kwa ukaribu
suala zima la Tender ya Ujenzi wa Barabara ya Uchira-Kisomachi, iliwa ni pamoja
na kujadiliana na Diwani. Pia kuimarisha nafasi ya LEKIDEA katika mchakato
mzima wa Mradi kabla haujaanza. Pia kuiwezesha LEKIDEA iwe kinywani mwa kila
Mwana-KV Mashariki ili kuhakikisha maendeleo yanawahusisha wote.
·
Mikakati Katika Kuuanza Mwaka Mpya:
§
Fund
Raising ya LEKIDEA
Kikao
kilipendekeza kuwa ipangwe mapema mwezi February, na siku rasmi itangazwe
katika vyombo mblimbali vya habari, makanisani na katika mitandao.
§
Ada ya Kudumu ya Wana-LEKIDEA:
Kikao
kilipendekeza kuweka kiwango kidogo cha Ada
kwa wanachama wote ili kuendesha Taasisi yetu, na ilipendekezwa Ada
isizidi Tsh 20,000/-. Mjumbe mmoja alishauri kuwa kutokana na wanachama kuwa
wengi, kiasi cha Tsh 1,000/- kikatosha
§
Mapendekezo Mengineyo:
Katika
kuendelea kuangalia vyanzo vya fedha vya kudumu, tuangalie pia uwezekano wa
kutumia njia ya kutuma neno fupi (short-code) kama kuchangia kwa makato
kidogo ya SMS au upigapo simu, iliafikiwa na itafuatiliwa na Ndg Paul Msaki,
kikao kiliafiki juhudi ziendelee.
Kikao
kilipendekeza pia kila mwana-LEKIDEA aweze kuitumia BLOG yetu ipasavyo, na wana LEKIDEA walio na miradi waweze
kutangaza biashara husika au fani zao mbalimbali katika Blog yetu ili
kuhakikisha kila mwana LEKIDEA na wale wasio wana-LEKIDEA, wanahamasika,
wanaipenda na kuitumia kujitangaza, Mfano Mabenki, Makampuni ya Simu nk.
§
Ilishauriwa
pia tuweze kuwatumia wana -LEKIDEA wenye uwezo katika
uandaaji wa Report –Write-Ups katika masuala mbalimbali ya kijamii, na
kuwasilisha katika taasisi mbalimbali za kitaifa na kimataifa ili baadaye
Write-Ups hizo zikikubalika ziwezeshe kukusanya na kuelekeza wapenda
maendeleo watuchangie kuendeleza eneo letu. Hili liliafikiwa.
§
Ilishauriwa
kuwa uzoefu unaonyesha Wafadhili
wanaziamini zaidi Taasisi za Kiraia (NGOs), hivyo ni muhimu kuwatumia
Wafadhili baadhi ya Card, na pia zitengenezwe Bronchures kwa ajili ya
Wafadhili (Donors) na Write-Ups
ziandaliwe kwa ajili ya malengo yetu
na miradi ,kuanzia January 1/2012, pia
suala la mazingira ,maji na barabara na huduma nyingine kama tutakavyoona
yafaa.
§
Kikao kiliafiki kuwa Ndg Joseph Shewiyo
ataanza kuandaa write-Ups za mradi mbalimbali kwa ajili ya Wafadhili. Ndiye
atakayesimamia masuala yote ya mchakato huu pia. Kadhalika ilipendekezwa kuwa
Ndg Sylvester Matemu ataombwa kuchangia kuhusu uandaaji kwa upande wake pia.
§
Kadhalika,
ilipendekezwa kuwa tuweze kuweka katika mpangilio kuizindua LEKIDEA rasmi
katika Kanisa la Karmeli katika Sikuku ya Noel (Chrisimasi) ili viongozi
watambulishwe rasmi siku hiyo ikijumuishwa viongozi viongozi kuombewa.
§
Ilipendekezwa
kuwa eneo letu (Legho-Kirua) linao idadi nzuri ya
mapadre, ambao ni viungo muhimu sana popote walipo, na wengi wamejaliwa
kuwepo nje ya nchi, zipatikane emails
zao wote ili wapewe taarifa za kila siku na maendeleo ya LEKIDEA, na wao
waweze kutushauri au kutuchangia pale inapowezekana, jambo ambalo
liliafikiwa.
§
Kuimarisha Sekretariat: Katika kuzidi kukuza na kuimarisha
zaidi safu ya Sekretariat, Kikao kilipendekeza
Ngd Amani Beda Kyara awe mjumbe wa-Sekretariat,
atakayekuwa kati ya kikosi kazi hicho katika shughuli za kila siku na pia
kama kiungo kwa ajili ya kuhakikisha mipangilio ya utekelezaji wa LEKIDEA kwa
upande wa maeneo ya LEGHO yanakwenda ipasavyo. Hili liafikiwa.
7.
Kufunga/Kuahirisha Kikao:
Kikao
kilifungwa saa 4:30 usiku kwa sala.
|
||||||||||||||||||||||||
Katika
kuwakumbusha Wana-LEKIDEA katika kutoa michango yao, wasisite kutumia njia
zifuatazo:
|
||||||||||||||||||||||||
AKAUNTI
YA LEKIDEA: Bank: CRDB BANK Plc.:
Jina la A/C: LEGHO KIRUA DEVELOPMENT
ASSOCIATION
A/C No: 0152095786500
|
||||||||||||||||||||||||
SIMU
MKONONI ZA LEKIDEA:
§ Vodacom – MPESA: 0755 799 133
§ Tigo – TigoPESA: 0653 799 133
|
||||||||||||||||||||||||
MWISHO
|
||||||||||||||||||||||||
----------------------------
----------------------------
Mwenyekiti
Katibu
|
1 comment:
Tunaomba maoni na ushauri zaidi toka kwa kila mwana-LEKIDEA, pale inapowezekana. Karibuni zana!
Post a Comment