Ni fursa ya kipekee kuwa tena kukutana katika mawasiliano ya Mtandao wa Blog yetu, pamoja na kupita kitambo kidogo tangu kukamilika vyema kwa miradi yetu mbalimbali, na hasa mradi mkubwa wa Barabara za Vijiji vyetu. Ni katika kuendeleza mshikamano na hamasa zetu za kimaendeleo, hatuna budi kutokurudi nyuma katika harakati hizi ambazo ndio msingi wa heshima na kujitambua asili yetu na uzao wetu pasipo kujisahau kuwa maendeleo ni sisi wenyewe.
Ni katika kuendeleza mshikamano wetu bila kujali dini siasa, jinsia na hali ya mtu, na hata kuungwa mkono na serikali ngazi mbalimbali. Hii ni ktk kutambua juhudi zetu na hivyo kutuunga mkono katika nyanja mbalimbali za kijamii, kama inavyozidi kudhihirika katika taarifa ifuatayo. Ifuatayo ni TAARIFA TOKA KWA DIWANI wetu Ndugu ALEX UMBELLA kama inavyowasilishwa..wote tuipitie kwa umakini, . Taarifa hii pia inaambatana na BOQs za Ujenzi wa Barabara zetu (Uchira - Kisomachi, na Mabungo - Nganjoni hadi Legho) zinavyoendelea, pamoja na MPANGO MKAKATI 2010 - 2020 wa Kata yetu ya KV Mashariki.
Ni fursa kwetu wote leo hii tuone ni jinsi gani tulivyo na hazina kubwa ya kiuongozi, na viashiria vya maendeleo na mafanikio zaidi katika Kata yetu na hivyo kutokudumaa au kukata tamaa kutonana na fikra za wachache wanaovunja wengine moyo, bali tuhamasike, kuendeleza kwetu na maeneo yanayotuzunguka, tuungane zaidi na hasa katika huduma za kijamii.
Taarifa hizi pia nakala zilitumwa katika mtandao wa e-mail wa LEKIDEA. -----------------------------------------------------------------------------------------------------------------
TAARIFA YA DIWANI, BOQs ZA BARABARA
NA MPANGO MKAKATI WA KATA KIRUA VUNJO MASHARIKI - 2010-2020
Mh. Alex J. Umbella
Wapendwa wana LEKIDEA
Napenda
kuvunja ukimya na kuchukua fursa hii ya pekee kuwashukuru kwa jitihada maalum
mlizozitoa kwa ajili ya maendeleo ya Legho Kirua. Jitihada zilianza na ujenzi
wa Kanisa la Karmel hatimaye zikapata msisimko upya wakati wa ujenzi wa awamu
ya kwanza ya miundombinu ya barabara za Vijiji. Hapana shaka tukio hili la
ujenzi wa barabara lilivuta hisia nyingi toka kwa Jamii na taasisi
zinazotuzunguka hasa ndani ya LEKIDEA, huku baadhi ya watu wakihoji hatma na
azma tuliyojiwekea. Kwa vyovyote vile hatuna budi kumshukuru Mwenyezi Mungu kwa
kutuvusha na kutuondolea hofu kwenye changamoto za kisiasa na nyinginezo
zilizojitokeza na hatimaye kutupeleka kwenye Dira ya Maendeleo tuliyojiwekea.
Michango
iliyoelekezwa kwenye ujenzi wa barabara takribani milioni themanini imetujengea
heshima kubwa ndani ya jamii ya wanalegho na Mkoani na hasa ndani ya
Halmashauri ya Wilaya ya Moshi ambako nasimamia na kutetea masilahi ya wananchi
wa Kata ya Kirua Vunjo Mashariki. Ikumbukwe ujenzi wa barabara haukufanywa kwa
kificho, nilikaribisha timu ya Halmashauri ya Wilaya ya Moshi hususan
Mkurugenzi Mtendaji, Afisa Mipango na Mhandisi wa ujenzi kutembelea Kirua Vunjo
kuona ni jinsi gani kazi ilivyokuwa ikifanyika.
Kilichowavutia
na kuwashangaza ni matumizi ya mashine maalum za ujenzi wa barabara ambazo ni
nadra sana kuonekana Vijijini mf. Caterpillar, bulldozer, roller, excarator.
Nawashukuru sana kwa uhamasishaji uliofanywa na viongozi wa LEKIDEA kwani
wananchi wenye mashamba yanayopakana na barabara walionyesha ukomavu wa hali ya
juu katika kuyapokea mabadiliko.
Barabara
zilizochimbwa, kuwekwa moram na kushindiliwa kwa roller zimeweza kuhimili
vishindo vya mvua za masika zilizokuwa nyingi na kutikisa sehemu mbalimbali za
nchi kwa sababu hiyo, barabara za Madukani – Kilasanioni, Madukani – Kisanja,
Madukani – Kiwelewele (via kwa W. Matay), na Madukani – Mrumeni (kwa Mkoloni)
zimeweza kupitika kipindi chote cha mvua kwa magari na pikipiki. Kadhalika
kiwango cha usafi hasa wa viatu na mavazi kwa wananchi wetu kimepanda kipindi
cha mvua.
Zaidi ya
hayo ujenzi wa barabara uliotekelezwa na LEKIDEA umekuwa wa kiwango kikubwa
zaidi kuliko ujenzi ulifanywa na Serikali. Hii inathibitishwa na ukweli kwamba
barabara ya Uchira – Kisomachi iliyotengenezwa muda mfupi tu kabla ya kuanza
kwa ujenzi wa LEKIDEA iliharibika na kusababisha kukwama kwa magari eneo la
Mtemboni na Msufin. Eneo la Mbuyuni kwa Mtanzania lililorekebishwa na LEKIDEA
limebaki kuwa salama. Hili ni jambo ambalo LEKIDEA inapaswa kujivunia. Mhandisi
wa barabara (W) ameliona hili na wakandarasi wa barabara watatakiwa kuzingatia
viwango pindi wafanyapo kazi katika eneo letu.
Wapendwa wana LEKIDEA
Serikali
nayo haijawa mbali na juhudi zetu. Mtakumbuka kuwa miaka miwili iliyopita
barabara ya Uchira – Kisomachi ilikuwa mbaya sana, Serikali ilitoa
T.Shs.47,000,000/= kuirejesha mahali pake. Pia zilitolewa T.Shs.5,500,000/=
kutengeneza barabara ya Madukani – Kolaria. Hapo majuzi Serikali imetoa tena
T.Shs.46,550,000/= kwa mkandarasi JABEL INVESTMENT CO. LTD ya jijini Dar es
Salaam. Shughuli hii ya ujenzi ipo katika hatua ya “mobilization”. Hatuna budi
kujenga uhusiano naye atuhakikishie kazi nzuri na ya viwango! Naambatanisha
BOQS kwa kazi hiyo. Wakati huo huo Serikali imetoa T.Shs.9,300,000/= kwa
matengenezo ya barabara ya Nganjoni – Mabungo iliyopo kwenye Kata yetu. Napenda
kuwajulisha kuwa kwa tathmini niliyofanya Kata yetu inapata fedha nyingi toka
kwenye mfuko wa barabara kuliko Kata nyingi za Halmashauri ya Moshi! Zaidi ya
hayo barabara ya Kisomachi – Nganjoni – Masaera (Kilema) imeingizwa Serikalini.
Hii itatuwezesha kupanua uwezo wa soko la Kileuo badala ya kumtafuta mchawi.
Serikali
imetoa T.Shs.55,000,000/= kwa ajili ya maendeleo ya Shule ya Sekondari Kilimani
chini ya mpango wa TASAF kutokana na fungu hilo Shule imeweza kununua madawati
100, viti 100, kabati za kuhifadhi vifaa, kujenga madarasa mawili na vyoo vya
wanafunzi. Hata hivyo, madarasa yamekamilika kwa shida na vyoo kujengwa bila
mfumo wa maji kutokana na kamati ya usimamizi (Mero) kutowajibika ipasavyo. Kwa
vyovyote vile udhaifu uliojitokeza unaanzia kwa wataalamu wachache wasiokuwa
waadilifu ndani ya Halmashauri ya Moshi. Tunafuatilia tatizo hili kwa karibu.
Jengo la
Zahanati ya Kileuo lililokuwa limeanza tangu mwaka 2007 na kuzuiliwa kwa miaka
kadhaa kutokana na usimamizi duni wa Serikali ya Kijiji, mkakati wa ujenzi wa
Zahanati umepata msukumo upya baada ya Serikali kutuma tena T.Shs.20,000,000/=
kwa masharti mapya chini ya uangalizi wa Kata. Tunatarajia kukamilisha ujenzi
mwaka huu na tayari tumeshaingiza Zahanati kwenye mpango wa huduma za Serikali.
Zahanati ya Kileuo imekuwa kikwazo kikubwa kwa ujenzi wa Ofisi ya Kata.
Tumeendelea
kuhamasisha bustani za miche ya kahawa kwa ajili ya wakulima wetu.
Msimu huu
chama chetu cha (KNCU) kimeweza kuzalisha miche 15,000 na kusambaza kwa
wakulima wetu. Bei ya mche mmoja ni shilingi 300. Miche mingi iitolewa kwa
mkopo kutokana na hali mbaya kifedha. Wakulima kadhaa wameanza kunufaika na
matunda ya miche bora ya kahawa ijapokuwa bei ya kahawa imeshuka kwenye soko la
dunia.
Tatizo la
ukosefu wa ajira kwa vijana wetu limekuwa kwa kiasi kikubwa na limeanza
kutishia maisha ya watu katika eneo letu. Kwa zaidi ya mwezi mmoja sasa uongozi
wa Kata umewakusanya na kuwaunganisha vijana katika vikundi vya watu kuanzia 10
hadi 25. Tumewafundisha namna ya kuandika katiba ya vikundi na kutengeneza
andiko la miradi na hivi karibuni tumetuma maombi ya mikopo Serikalini ili
vijana waweze kunufaika na fungu la Maendeleo ya Vijana. Kutokana na mkakati
huu vijana wameweza kujitambua ndani ya jamii na wengine wameweza kunyoosheana
vidole pale ilipobidi kufanya hivyo. Tunasubiri tuone mwisho wake.
Hapana
shaka kuwa mikakati ya kimaendeleo iliyoanzishwa LEKIDEA imeleta changamoto
mbalimbali katika historia ya maendeleo Kirua Vunjo. Kutokana changamoto hizi,
zimejitokeza harakati mbalimbali ambazo zimeanza kukabili viongozi ambao
wameshindwa kuendana na mahitaji ya sasa ya wanachi. Viongozi / Watumishi
walevi, wazembe wsio waadilifu, wameanza kukumbana na kadhia hii. Tayari
Mwenyekiti wa Kijiji cha Mrumeni amekumbwa na karaha hii. Wimbi linaendelea na
hakuna anayejua mwisho wa siku litakuwaje. Cha msingi ni mabadiliko chanya.
Naomba
nisiwachoche sana kwa mawazo yangu nikaribishe hoja mbalimbali kwa ajili ya
kupambana na changamoto zetu za kimaendeleo katika eneo letu. Mungu aendelee
kuwajalia afya na uzima.
Alex J.
Umbella
DIWANI
Kata ya Kirua Vinjo Mashariki.
Aug 2013
Bil of Quantities for Uchira - Kisomachi Road -
7Km
|
||||||
Spesc
|
||||||
S/n
|
Eescription
of Work
|
Ref
|
Unit
|
Qty
|
Rate
|
Amount
|
1
|
Part
A.Preliminary ang General Items
|
|||||
1.1
|
Mobilization?Demobilization
|
1.2
|
Lsum
|
1
|
3,000,000.00
|
3,000,000.00
|
1.2
|
Provision
sum for erection of sign
|
|||||
board
|
1.6
|
Lsum
|
1
|
6,000,000
|
6,000,000
|
|
1.3
|
Field
compaction test and
|
|||||
laboratory
material testing
|
1.5
|
Lsum
|
1
|
1,000,000
|
1,000,000
|
|
Sub
Total Part . A
|
4,600,000
|
|||||
2.0
|
Part
BOAD WORKS
|
|||||
2.1
|
Site
clearance (grass cutting)
|
2.1
|
m²
|
3000
|
300
|
900,000
|
2.2
|
Light
reshaping
|
2.7.2
|
km
|
5
|
1,400,000
|
7,000,000
|
2.3
|
Excavate,
Load, haul, spread,
|
|||||
water
and compact gravel
|
||||||
wearing
course 150mm think to
|
||||||
the
required density (95%Mdd)
|
2.8
|
m³
|
1350
|
22,000
|
29,700,000
|
|
3.0
|
Sub
Total Part . B
|
37,600,000
|
||||
3.1
|
Part C.
Drainage Works
|
|||||
Repair
head walls and disilting
|
||||||
of
concrete pipe culverts 600mm
|
||||||
diameter
|
4.4
|
Nos
|
4
|
100,000
|
400,000
|
|
3.2
|
Re-excavate
mitre drains
|
5.1.5
|
m
|
300
|
1,500
|
450,000
|
Construction
of stone masonry
|
||||||
line
ditches
|
5.14
|
m
|
70
|
50,000
|
3,500,000
|
|
Sub
Total Part . C
|
4,350,000
|
|||||
GRAND
TOTAL (A+B+C)
|
46,550,000
|
|||||
Bill of Quantities for Nganjoni - Mabungo Road
4.5km
|
||||||
S/n
|
Eescription of Work
|
Spesc Ref
|
Unit
|
Qty
|
Rate
|
Amount
|
1.0
|
Part
A.Preliminary ang General Items
|
|||||
1.1
|
Mobilization
/ Demobilization
|
1.2
|
Lsum
|
1
|
1,000,000
|
1,000,000
|
Sub
Total Part .A
|
1,000,000
|
|||||
2.0
|
Part B.
ROAD WORKS
|
|||||
2.1
|
Site
clearance (grass cutting)
|
2.1
|
M²
|
1500
|
300
|
450,000
|
2.2
|
Light
reshaping
|
2.7.2
|
KM
|
3.5
|
1,400,000
|
4,900,000
|
2.3
|
Sport
graveling
|
2.3.3
|
M³
|
50
|
17,000
|
859,000
|
Sub
Total Part . B
|
6,200,000
|
|||||
3.0
|
Part C.
Drainage Works
|
|||||
3.1
|
Re-excavate
mitre drains
|
5.1.4
|
M
|
100
|
1500
|
150,000
|
3.2
|
Repair
head walls and disilting
|
4.4
|
Nos
|
2
|
30,000
|
60,000
|
of
concrete pipe culverts 600mm
|
||||||
diameter
|
||||||
3.3
|
Suplply
and fix concrete pipe t
|
|||||
culvert
including inlet and outlet
|
||||||
drains,
150mm thick concrete
|
||||||
sorroundings
grade 20, stone
|
||||||
masonry
headwall, wing wall and
|
||||||
sprons.
|
||||||
a.
600mm dia concrete culverts
|
5.3
|
m
|
7
|
270,000
|
1,890,000
|
|
Sub
Total Part C.
|
2,100,000
|
|||||
GRAND
TOTAL
|
9,300,000
|
|||||
GRAND
TOTAL SUMMARY
|
||||||
1
|
PRELIMINARY
AND GENERAL ITEMS
|
TSHS.
|
7,600,000
|
|||
2
|
UCHIRA
- KISOMACHI
|
TSHS.
|
41,950,000
|
|||
3
|
KAWAWA
- YAMU - NDUONI
|
TSHS.
|
7,850,000
|
|||
4
|
UCHIRA
- MIWALENI - KISANGESANGENI
|
TSHS.
|
10,340,000
|
|||
5
|
NGANONI
- MABUNGO
|
TSHS.
|
8,300,000
|
|||
GRAND
TOTAL SUMMARY
|
TSHS.
|
76,040,000
|
||||
---------------------------------------------------------
MPANGO MKAKATI WA KATA 2010-2020
MPANGO MKAKATI WA
MAENDELEO KATA KIRUA VUNJO MASHARIKI 2010 - 2020
|
||||
SEKTA
|
LENGO
|
UTEKELEZAJI
|
MHUSIKA
|
VIASHIRIA
|
|
|
|
||
|
Kuinua kiwango cha maisha cha
|
|
|
|
|
wakazi wa Kata ya Kirua Vunjo
|
|
|
|
|
Mashariki ifikapo mwaka 2020.
|
|
|
|
|
|
|
|
|
UONGOZI
|
Jamii iweze kujisimamia yenyewe
|
> Kujenga uwezo wa:-
|
DIWANI /
|
> Uwepo
wa Viongozi wanaoelewa
|
|
kwa ajili ya maendeleo endelevu.
|
|
MKURUGENZI
|
majukumu yao.
|
|
(i)
Viongozi wa Vijiji.
|
|
||
|
|
>
Watendaji / Watumishi wenye
|
||
|
(ii)
Watendaji wa Vijiji
|
mipango kazi.
|
||
|
na
Kata.
|
|
||
|
|
>
Vikao vya Serikali ya Vijiji
|
||
|
(iii) Watumishi wa umma
|
kufanyika kisheria.
|
||
|
ngazi
ya Vijiji na Kata.
|
|
||
|
|
>
Mikutano Mikuu ya Vijiji inafanyika.
|
||
|
(iv) Wenyeviti wa Vitongoji
|
|
||
|
wamudu kutekeleza
|
>
Ushiriki wa wananchi katika Uongozi.
|
||
|
majukumu yao ya kila
|
|
||
|
siku.
|
>
Jamii inachangia maendeleo yao.
|
||
|
|
|
||
|
>
Kuhamasisha wananchi
|
AFISA MAENDELEO
|
>
Vikundi vya wafugaji, biashara ndogo,
|
|
|
waweze
kutambua haki
|
JAMII
|
ndogo
wakulima hasa vya Vijana.
|
|
|
zao za
msingi na kuwajibika
|
|
|
|
|
ipasavyo.
|
|
|
|
|
|
|
|
|
|
>
Kuunda vikundi vidogo
|
|
|
|
|
vidogo
vya uzalishaji
|
|
||
|
mali
(IGAs)
|
|
||
|
|
|
||
|
>
Ujenzi wa Ofisi ya Kata
|
DIWANI /
|
>
Ofisi mpya.
|
|
|
|
MKURUGENZI
|
|
|
|
|
MTENDAJI (W)
|
|
|
|
|
|
||
|
|
|
|
|
SEKTA
|
LENGO
|
UTEKELEZAJI
|
MHUSIKA
|
VIASHIRIA
|
|
> Kuunda
upya Benki ya Akiba
|
> Watu
wanaoweka na
|
||
|
na
Mikopo
|
kuchukua fedha.
|
||
|
(Kirua
Vunjo East SACCOS)
|
|
||
|
|
>
Mikopo ikiidhinishwa na
|
||
|
|
kurejeshwa.
|
||
|
|
|
|
|
KILIMO NA
|
Kuboresha na kuimarisha
|
>
Kuanzisha na kuendeleza
|
DIWANI /
|
>
Uwezo wa bustani za
|
UFUGAJI
|
upatikanaji wa chakula katika
|
mifereji ya asili kwa ajili
|
AFISA KILIMO
|
mboga
na ustawi
|
|
ngazi ya Kaya.
|
ya
umwagiliaji.
|
wa
mashamba ya
|
|
|
|
uzalishaji mali
|
||
|
>
Kutoa mafunzo kwa wakulima
|
yasiyotegemea mvua
|
||
|
wadogowadogo Kuhusu mbinu bora
|
kwa
100%.
|
||
|
za
uzalishaji.
|
|
||
|
|
|
||
|
>
Kujenga uhusiano hai kati ya
|
>
Upatikanaji wa aina
|
||
|
maendeleo na watoto.
|
mbalimbali za lishe, pia watoto
|
||
|
|
kwa
ridhaa yao wapewe nafasi
|
||
|
|
ya
kufuga wanyama wadogo wadogo
|
||
|
|
kama
- sungura, visili, kuku n.k.
|
||
|
>
Kuanzisha / Kuendeleza
|
|
||
|
shughuli za uhifadhi wa ardhi
|
|
||
|
na
kuboresha vyanzo vya maji.
|
>
Uwepo wa bustani za
|
||
|
|
miti,
ili kutunza asili ya maeneo yetu.
|
||
|
>
Kuanzisha bustani mama na
|
>
Vyanzo vya maji vilivyo-
|
||
|
kuendeleza bustani zilizopo
|
pandwa
miti.
|
||
|
kukuzia miche bora ya kahawa.
|
|
||
|
|
|
||
|
>
Kuboresha mifugo m.f. ngombe,
|
>
Usambazaji wa miche
|
||
|
mbuzi,
kuku wa kienyeji na hata wa
|
|
bora
ya kahawa kwa
|
|
|
kisasa.
|
|
mkulima mmoja mmoja.
|
|
|
|
|
|
|
|
|
|
>
Kituo cha uhamilishaji
|
|
|
|
|
|
|
|
|
|
|
|
|
|
>
Upatikanaji wa mifugo
|
||
|
|
|
|
bora.
|
SEKTA
|
LENGO
|
UTEKELEZAJI
|
MHUSIKA
|
VIASHIRIA
|
|
|
|
|
|
ULINZI NA
|
Ustawi wa Ulinzi na Usalama
|
>
Kuanzisha kikosi Kata cha
|
DIWANI /
|
>
Ufuatiliaji wa kudumu wa
|
USALAMA
|
wa raia na mali.
|
wanamgambo kwa ajili ya
|
MTENDAJI KATA
|
uhalifu.
|
|
|
ulinzi
na usalama wa raia na
|
|
|
|
|
mali
zao.
|
|
|
|
|
|
|
|
|
|
>
Kutoa mafunzo kwa kikosi cha
|
|
>
Uhalifu kupungua.
|
|
|
wanamgambo kwa kila Kijiji.
|
|
|
|
|
|
|
|
|
|
>
Kujenga dhana ya ufahamu
|
|
>
Mawasiliano chanya kati
|
|
|
wa
uhalifu baina ya raia.
|
|
ya
raia na Viongozi.
|
|
|
|
|
|
|
|
>
Kutengeneza mazingira ya kila
|
|
>
Upatikanaji wa sheria
|
|
|
mwenye
uwezo wa kufanya
|
|
ndogondogo dhidi ya
|
|
|
kazi awajibike ipasavyo.
|
|
uzururaji, ulevi, matusi n.k
|
|
|
|
DIWANI
|
|
|
|
>
Ujenzi wa kituo cha Polisi na
|
LEKIDEA
|
>
Uwepo wa Kituo cha Polisi Kata
|
|
|
Mahakama.
|
MKURUGENZI
|
na
Baraza la usuluhishaji.
|
|
|
|
|
|
|
|
|
|
|
|
|
|
|
|
SEKTA
|
LENGO
|
UTEKELEZAJI
|
MHUSIKA
|
VIASHIRIA
|
|
|
|
||
ELIMU
|
Kutoa elimu bora kwa watoto wa
|
>
Ujenzi wa miundombinu ya
|
DIWANI / MRATIBU
|
>
Kupungua kwa watoto
|
|
umri wa kwenda shule.
|
kutosheleza k.v. madarasa, jiko,
|
ELIMU KATA
|
wazururaji mitaani.
|
|
stoo,
vyoo na viwanja vya
|
AFISA ELIMU (W)
|
|
|
|
michezo katika shule za msingi.
|
|
>
Mahudhurio kuongezeka.
|
|
|
|
|
|
|
|
>
Ujenzi wa miundombinu
|
|
>
Michezo kufanyika mashuleni.
|
|
|
inayohitajika katika shule za
|
|
|
|
|
sekondari k.v. madarasa, maktaba
|
|
>
Ufaulu wa shule za
|
|
|
maabara, vyoo na nyumba za
|
|
sekondari kuongezeka.
|
|
|
walimu.
|
|
|
|
|
|
|
>
Upatikanaji wa vitabu,
|
|
|
>
Uzambazaji wa vifaa vya
|
|
samani
nyingine ambazo ni muhimili
|
|
|
kufundishia katika shule za
|
|
wa
Elimu.
|
|
|
msingi na sekondari.
|
|
|
|
|
|
|
>
Kiwango cha mahudhurio
|
|
|
>
Kuhamasisha walimu na
|
|
ya
walimu kuongezeka.
|
|
|
kurejesha nidhamu ya kiutendaji
|
|
|
|
|
|
|
|
|
|
> Kuhamasisha wazazi /
|
|
>
Upatikanaji wa chakula
|
|
|
wananchi kutambua jukumu la
|
|
cha
mchana mashuleni.kufuta dhana
|
|
|
kuchangia elimu.
|
|
kwamba Elimu ni sehemu ya ukuaji
|
|
|
|
|
kwa
kuhamasisha jinsi ya kutumia
|
|
|
|
|
utajiri wa fikra kuleta ukombozi wa
|
|
|
|
|
maisha.
|
|
|
|
|
|
|
|
|
|
|
|
SEKTA
|
LENGO
|
UTEKELEZAJI
|
MHUSIKA
|
VIASHIRIA
|
|
|
|
||
AFYA
|
Kuinua kiwango cha afya ya
|
>
Kuhamasisha wanajamii kujenga
|
DIWANI
|
>
Ongezeko la vyoo bora.
|
|
msingi ya Jamii.
|
vyoo
bora katika kila Kaya.
|
AFISA AFYA
|
|
|
|
|
|
|
|
>
Kufanikisha zoezi la chanjo kwa
|
|
>
Takrimu za chanjo kuongezeka.
|
|
|
watoto
wa umri chini ya miaka mitano.
|
|
|
|
|
|
|
|
|
|
>
Ujenzi wa vituo vya tiba na upatikanaji
|
|
>
Uundaji wa kamati za afya
|
|
|
wa
dawa za tiba.
|
|
zinazofanya kazi.
|
|
|
|
|
|
|
|
>
Kusimamia zoezi la usafi binafsi na
|
|
>
Taarifa za ukaguzi.
|
|
|
usafi
wa mazingira majumbani.
|
|
|
|
|
|
|
|
|
|
>
Kusimamia zoezi la usafi wa maeneo
|
|
> Ukaguzi
wa vyanzo unafanyika
|
|
|
umma
k.v. mashuleni, vilabuni, sokoni,
|
|
siku
hadi siku.
|
|
|
vituo
vya tiba na machinjio.
|
|
|
|
|
|
|
|
|
|
>
Kuanzisha na kuendeleza michezo.
|
|
>
Vijana wanaojishughulisha na michezo
|
|
|
|
|
kama moja
ya burudani.
|
|
|
|
|
|
|
|
|
|
|
|
|
|
|
|
|
SEKTA
|
LENGO
|
UTEKELEZAJI
|
MHUSIKA
|
VIASHIRIA
|
|
|
|
||
UKIMWI
|
Kusia mbegu ya matumaini kwa
|
>
Kuunda kamati za UKIMWI ngazi za
|
AFISA MAENDELEO
|
>
Wagonjwa na waathirika
|
|
wagonjwa na waathirika wa
|
Vijiji
na Kata.
|
JAMII / DIWANI
|
wanatembelewa.
|
|
UKIMWI na magonjwa sugu.
|
AFISA AFYA
|
|
|
|
|
>
Kuanzisha mfuko wa huduma kwa
|
|
>
Dawa, chakula, nguo vinatolewa
|
|
|
wagonjwa na wanaoishi na virusi vya
|
|
kwa
wahusika.
|
|
|
UKIMWI
|
|
> Watoto waathirika / yatima wanalipiwa
|
|
|
|
ada
shuleni.
|
|
|
|
|
|
|
|
|
>
Waathirika wanawezeshwa kwa lengo
|
|
>
Miradi ya mbuzi wa maziwa.
|
|
|
la
kujitegemea.
|
|
>
Bustani za mbogamboga.
|
|
|
|
>
Ustawi wa biashara ndogondogo
|
|
|
|
|
kwa
waathirika.
|
|
|
|
|
|
|
|
|
>
Kutoa elimu kwa Jamii.
|
|
>
Mabadiliko ya tabia yenye kujenga
|
|
|
|
amali
na tunu bora za ukuaji na
|
|
|
|
|
upambanaji dhidi ya mazingira
|
|
|
|
|
hatarishi. Upendo kuelekezwa kwa
|
|
|
|
|
wahanga
wa moja kwa moja na
|
|
|
|
|
wagonjwa.
|
|
|
|
|
|
|
|
|
|
|
|
|
|
|
|
|
SEKTA
|
LENGO
|
UTEKELEZAJI
|
MHUSIKA
|
VIASHIRIA
|
|
|
|
|
|
Mawasiliano
|
Kuboresha maendeleo ya
|
>
Ujenzi na upanuzi wa barabara za
|
DIWANI
|
>
Barabara zinapitika majira yote kwa
|
na Nishati
|
miundombinu ya mawasiliano na
|
LEKIDEA
|
mwaka.
|
|
|
nishati
|
(i)
Uchira - Kisomachi - Kolaria.
|
MKURUGENZI
|
|
|
|
|
>
Upatikanaji wa usafiri mbadala.
|
|
|
|
(ii)
Kisomachi - KNCU - Kilasanioni.
|
|
|
|
|
|
>
Ongezeko la bidhaa na
|
|
|
|
(iii)
Kisomachi - Kiwelewe - Lasso.
|
|
wafanyabiashara katika soko la
|
|
|
|
Kileuo.
|
|
|
|
(iv) KNCU
- Sumi.
|
|
|
|
|
|
|
|
|
|
(v)
Kisomachi - Nganjoni - Masaera.
|
|
|
|
|
|
|
|
|
|
(vi)
Mabungo - Nganjoni - Legho Kilema.
|
|
|
|
|
|
|
|
|
|
(vii)
Kilasanioni - Kwamaambo - Iwa.
|
|
|
|
|
|
|
|
|
|
>
Kuboresha kiwango cha mitandao ya
|
|
>
Ujenzi wa minara ya mawasiliano .
|
|
|
mawasiliano k.m. voda, airtel na tigo.
|
|
|
|
|
|
>
Mawasiliano angavu .
|
|
|
|
>
Ujenzi wa miundombinu ya nishati ya
|
|
|
|
|
umeme.
|
|
>
Upatikanaji wa umeme Kileuo Kusini
|
|
|
|
na
Nganjoni.
|
|
|
|
|
|
|
|
|
|
>
Ongezeko la watumia umeme.
|
|
|
|
|
|
|
NB. Umeandaliwa na Alex J. Umbella na
kupitishwa na Kamati ya maendeleo ya Kata - K..V. mashariki
|
NOTE:
SEKRETARIAT
YA LEKIDEA, BAADA YA KUVUTA PUMZI KIDOGO KUTOKANA NA MAJUKUMU MENGINE
YA KIJAMII YALIYOKUWA HAYAEPUKIKI, HIVI KARIBUNI ITAENDELEZA TENA
MAJUKUMU YAKE RASMI KWA SPEED NA UMAHIRI MKUBWA KAMA AWALI KUANZIA MWEZI
UJA. KAMA TAARIFA ILIVYOKWISHATOLEWA NA MAKAMU-KATIBU WA LEKIDEA, NDG
MARTIN M. KESSY.
TUNASONGA MBELE NA DAIMA TUTAFANIKIWA: TUUNGANE MIKONO.
Wenu;
SEKRETARIAT - LEKIDEA.