LEKIDEA FOCUS OVERVIEW

LEKIDEA
is a registered Non-profit Organization of Kirua Vunjo East Moshi, by Natives from related Villages (Kileuo, Mrumeni, Kotule, Mero, Legho, Lasso, Kwa-Laria(Kanji), dedicated to join together, leverage their Vision, Objectives, Social strengths, ambitions & professionalism and other common resources from members, relatives and families having any origination with K.V East, to come TOGETHER, DEVELOP and CHANGE their Motherland through Projects and involvements in different Social development Initiatives that play roles in alleviating poverty and enhancing opportunities in collaboration with all well wishers, and support from social development entities from the village level, national level, and international level.

Monday, December 10, 2012

LEKIDEA: KIKAO CHA TATHIMI YA MIRADI, DIRA 2013, UJUMBE WA M/KITI

IFUATAYO NI TAARIFA FUPI YA KIKAO CHA TATHMINI YA MIRADI, 2012, NA DIRA MPYA 2013.
-------------------------

KIKAO CHA LEKIDEA


KUTATHMINI MIRADI YA LEKIDEA
NA DIRA YA MWAKA MPYA 2013

Venue: DOUBLE VIEW HOTEL, SINZA – DSM.
Date: 02/12/2012

MINUTES ZA KIKAO

AGENDA

1. Writeups: Food Aid & JICA nk.
2. Media Conference na Statement kwa Wana-LEKIDEA na Umma wote.
3. Programme na Dira ya Mwaka Mpya 2013.
4. Ada ya Kila Mwana-LEKIDEA na Manufaa yake.
5. Mengineyo

MCHANGANUO WA AGENDA

Kufungua Kikao:
Kikao kilifunguliwa saa 12:00 jioni kwa sala.

1.      Writeups: Food Aid & JICA:
Ø  Kikao kiliafikiana kuwa Katibu, Ndg Joseph Shewiyo ataandaa Draft ya Writeups na kuiwasilisha kwa Sekretariat ambayo itaipitia, kuijadili na kuikamilisha mapema kwa ajili ya kusambaza ktk taasisi mbalimbali ikiwa ni pamoja na Food Aid na JICA ili kutafuta ufadhili wao kwa miradi ijayo ya LEKIDEA.

2.      Report ya Sekretariat kwa Wana-LEKIDEA na Umma
Ø  Sekretariat iliwasilisha taarifa kwa ufupi kuhusu mradi wa barabara ulivyokwisha kufikia hadi sasa, na malengo yajayo ili kuhakikisha kuwa tuna maendeleo endelevu.
Ø  Kikao kiliafiki kuwa iandaliwe Taarifa rasmi (Media Statement) ya jumla, itakayounganisha ile Taarifa kwa Umma iliyotoka awali pamoja na Taarifa mpya ya mwaka mpya itakayotoka hivi karibuni, ili iwasilishwe kwa vyombo vya Habari katika mipangilio ifuatayo:
ü  Katibu kuandaa makala ili itolewe kwenye vyombo vya habari.
ü  Iandaliwe Taarifa iliyokamilika vyema (Media Statement), ikionyesha Profile ya LEKIDEA na miradi yake na mafanikio hadi sasa.
ü  Taarifa hii pia itaunganisha taarifa ya awali iliyotolewa kwa Vyombo vya Habari, pamoja na taarifa mpya ya Mwaka Mpya 2013, pamoja na picha za wananchi na Miradi ilivyokuwa inafanywa, na Video za kazi zilivyokuwa zikiendelea.
ü  Mh Diwani Alex Umbella aliahidi kuwasilisha video za matukio hayo ili ziweze kutumika ktk kuandaa Media Conference hiyo.
ü  Tukio hili litawasilishwa na M/Kiti, pamoja na Katibu au Kaimu Katibu, ktk Ukumbi wa HABARI MAELEZO, na maandalizi yanafanyika ili iweze kufanyika kabla ya Tarehe 15/12/2012.

3.      Programme Kubwa na Dira ya Mwaka Mpya 2013:
Ø  Kikao kiliafiki kuwa katika kuendeleza malengo ya mafanikio ya wananchi wetu, LEKIDEA imeainisha malengo na mipango kabambe kwa Mwaka Mpya 2013 kama ifuatavyo:
ü  Kumalizia ujenzi wa barabara kwa kujenga culverts na barabara ndogondogo za ndani, pia kuongezea moram sehemu zenye upungufu

ü  Kuanzisha vitalu vya miche ya miti hususan ya Mierezi (gravelia) ipatayo 10,000/- (elfu kumi) kwa kuanzia ambayo itatolewa kwa wanavijiji ili wapande katika maeneo mbalimbali ya ukanda wetu ikijumuisha kando ya barabara zetu, na ktk kingo za mashamba.
ü  Mhe Diwani atafuatilia ufufuaji na uendelezaji wa bwawa la Urenga kwa kuhimiza Halmashauri ya Wilaya ilifufue na kuliendeleza kwa ajili ya umwagiliaji.  Hili litawezesha wananchi wetu kufaidika na Samaki, na umwagiliaji wa Mboga na mazao mengineyo.
ü  Harambee ya kuchangisha hela za maendeleo ya miradi ya Lekidea  kufanyika ndani ya Februari 2013 ili kuwahi mvua za Masika kwa ajili ya Moram, Maintenance ya Njia na Coverts nk.

4.      Ada ya Kila Mwana-LEKIDEA
Ø  Kikao kiliafiki kuwa ili kuwezesha taasisi yetu iweze kusonga mbele kwa mafanikio na kuwatumikia wananchi pasipo kukwama popote, kila mwana-LEKIDEA na mpenda-maendeleo atatoa ada ya kudumu ya Sh 100,000/- (Laki moja) kwa mwaka, ada ambayo itakuwa nyezo kwa LEKIDEA na Malengo yake ya muda mrefu LEGHO-KIRUA ikiwa ni pamoja na utekelezaji wa yafuatayo:-
ü  Lengo kuu; Kuendeleza, Kusimamia (Maitenance) Barabara zetu zote kwa kipindi chote cha mwaka mzima.
ü  Lengo jingine; Ada hii pia itatumika kama sehemu ya uchangiaji wa masuala ya maendeleo endelevu ya Legho-Kirua na hivyo LEKIDEA itatambua na kuthamini sana nafasi na kipaumbele cha mchangiaji katika kushirikiana naye masuala ya kijamii.
ü  Manufaa kwa Mtoa Ada: Kutokana na umuhimu wa kuwezesha maendeleo yetu kuwa endelevu, LEKIDEA itamtambua na kumthamini kila mtoa ada ya uanachama kwa kuhamasisha wengine kushirikiana naye katika masuala muhimu ya kijamii atakayokabiliana ikiwa ni pamoja na matukio kama Misiba, Harusi, Magonjwa nk.
ü  Madhara ya Kutokutoa ada; Wapo wazaliwa wa Legho-Kirua ambao mbali na kusikia, kuhamasishwa na kusukumwa sana kuchangia maendeleo na miradi yetu, wamekuwa wagumu sana, wengine wakibeza, na kudharau juhudi hizi, na pia wengine kuwakwaza wengine ili tu kuwakatisha tamaa wasichangie umoja huu. Huu ni mwenendo usiokubalika.
ü  Hivyo basi, kulingana na umuhimu wa ada hii kwa maendeleo ya jamii yetu, mwananchi atakayekwamisha au kushindwa kuunga mkono na kutoa ada hii kwa malengo yasiyo dhahiri, au kwa visingizio visivyoeleweka, wakati ukweli ni kuwa, ameshafaidika na anafaidika kwa sasa na ataendelea kufaidika na jasho la wengine wapenda maendeleo wa Legho-Kirua waliokwisha kuchangia kwa hali na mali, taasisi ya LEKIDEA haitamvumilia mtu wa mwenendo huo, na haitasita kumfichua, na pia kuwafahamisha wanachama na wananchi wote wapenda maendeleo wa Legho-Kirua ili watambue mwenendo wa mtu husika, na hata ikiwezekana, LEKIDEA itachukua jukumu la kwanza kuhamasisha pale inapowezekana ili mwananchi kama huyo asiweze kuungwa mkono, au kuchangiwa katika masuala ya kijamii kama misiba, harusi, magonjwa nk. ‘Asiyeotesha nawe hawezi kuvuna nawe’

5.      Mengineyo
Ø  Lobbying: Kikao kilipendekeza uwepo mpango wa kukutana na Engineer wa Manispaa kwa Mazungumzo ya Maendeleo yetu, hasa kuhusu budgets allocation, hasa ktk mifereji ya maji ambayo ni kati ya chaguo letu kubwa ktk maeneo ya utekelezaji.

Kikao kilifungwa saa 3:45 usiku kwa sala.

HAHUDHURIO:
1.       Eng Simon T Njau - Makamu/MKti
2.       Joseph I Shewiyo - Katibu
3.       Martin M Kessy - Makamu/Katibu
4.       Mh Alex Umbella - Diwani wetu
5.       Emilia J Saluo - Mwanasekretariat
6.       Paul Z Msaki - Mwanasekretariat
7.       Stephen Vendelin Msacky - Mjumbe
8.       Dr Kessy, Mkoloni - Mjumbe

UDHURU:
1.       Edward F Msaky - M/Kiti
2.       Eng Bernard D. Ndepachio - Mwanasekretariat.
3.       Aman Beda Kyara
4.       Venance Vendelin Msacky



--------------------                                               ----------------------
Katibu                                                                                M/Kiti

Katika kuwakumbusha Wana-LEKIDEA katika kutoa michango yao, wasisite kutumia njia zifuatazo:
AKAUNTI YA LEKIDEA:        Bank: CRDB BANK Plc.:
Jina la A/C:   LEGHO KIRUA DEVELOPMENT ASSOCIATION
A/C No:   0152095786500
SIMU MKONONI ZA LEKIDEA:       
§  Vodacom – MPESA:  0755 799 133
§  Tigo – TigoPESA: 0653 799 133
MWISHO


-------------------------&&&&&---------------------------

HABARI ZA MAENDELEO YA KIRUA VUNJO MASHARIKI CHINI YA USIMAMIZI WA LEKIDEA KAMA ZILIVYORIPOTIWA NA MAGAZETI YA THE GUARDIAN NA NIASHE HIVI KARIBUNI.
 ---------------------------

UJUMBE NA SALAMU RASMI ZA MWENYEKITI WA LEKIDEA KWA AJILI YA X-MASS 2012 NA MWAKA MPYA 2013 KWA WATU WOTE 
 





Tuesday, November 20, 2012

LEKIDEA: KIKAO CHA HIVI KARIBUNI NA KAZI INAYOENDELEA KV




 LEGHO-KIRUA DEVELOPMENT ASSOCIATION

KIKAO CHA DHARURA CHA SEKRETARIAT NA UONGOZI WA LEKIDEA -26/10/2012

Double Views Hotel – Sinza DSM

KUTATHMINI HALI YA MAENDELEO YA BARABARA
 ------------------------------------------------------
Agenda
1.       Kufungua Kikao
2.       Hali ya Sasa – Current situation
3.       Hatua zinzofuata - Way Forward
4.       Barabara ndogo za Vitongoji - Periphery Roads
5.       Uzinduzi  Rasmi wa Mradi
6.       Michango
7.       Mengineyo
 ------------------------------------------------------
1.       Kufungua kikao
-Kikao kilifunguliwa saa 1:30 jioni kwa sala na Ndg.Joseph Shewiyo – Katibu wa LEKIDEA.
2.       Taarifa ya Hali ya Sasa toka KV.
Utangulizi:
-Mwenyekiti  alianza kwa kuwashukuru wajumbe wote ambao tangu kuanzishwa kwa LEKIDEA hadi sasa wamekua wanajitoa kwa kila hali bila kuchoka na kuhakikisha miradi ya LEKIDEA inasonga mbele bila kukwama hasa katika ujenzi wa barabara, ugumu wowote unaotokea wanabuni mbinu mpya katika kukwamua. Aliwashukuru hususan Martin, Saluo, Shewiyo, Paul, na pia ma-engineer Benin na Njau. Alimalizia kuwa Mungu awabariki sana kwa uvumilivu na kujituma kwao kwa faida ya LEKIDEA na jamii nzima ya KV Mash.

3.  Taarifa Fupi toka KV:
Ø  Martin Kessy alitoa taarifa fupi ya hali ya uwekaji wa Moram iliyoanzia maeneo kadhaa ya Mradi wetu kama ituatavyo:
·         Kiwelewele hadi kwa Matay.
·         Kisanja hadi Kisomachi
·         Kilasanioni hadi kwa Kikuyu-Kitaarinyi
·         Mrumeni hadi Kisomachi.
·         Pendekezo lilitolewa kujumuisha ya njia ya kuanzia Kitaarinyi hadi Kisomachi

Ø  Jumla hadi siku ya kikao, idadi ya malori 200 yalikwishawekwa kwa gharama ya kiasi cha sh.24,000,000  ila zimelipwa trip 100 tu imebaki deni trip 100 ambayo katika Mil 24 zilizopo sasa kiasi cha Mil 12 kitatumika kulipia hayo malori 100. Tutabakiwa na  mil.12 ambazo zinatakiwa kufanya kazi ya kusambaza, kumwagia maji na kushindilia. Aidha zinatakiwa pia kumalizia maeneo matano muhimu ambayo ni barabara ya kutoka Uchira, Kitaarinyi hadi Kisomachi, Kiwelewele hadi Mkombenyi, Kitaarinyi hadi kwa Erene na KNCU Usangi hadi Kilasanioni  

4.       Hatua Inayofuata:
Ø  Kutokana na hali halisi, kiasi kilichosalia ni  12 mil. Michango zaidi inahitajika haraka ili kazi iendelee kwa kasi bila kusimama.
Ø  Zipo trip kama 24 katika hizo mia mbili ambazo bado hazijawekwa. Imeshauriwa kuwa tumkope mwenye Malori trip nyingine 50 ili zitoshe kuweka moram katika barabara zifuatazo ambazo bado:
·         Kitaarinyi kupitia Usangi  hadi Kilasanioni.
·         KNCU hadi kwa-Rene
·         Kwelewele hadi Lasso - Juu (Mkombenyi)
·         Kitaarinyi hadi Kisomachi
·         Kisomachi hadi Uchira (pale Juu ya Maweni na Kiorotsuni)

Ø  Pia imependekezwa  kuwa Doza  litengenezwe haraka ili kumalizia barabara za KNCU hadi Kwa-Rene na KNCU hadi Usangi -Kilasanioni

Boza, Greda na Compactor: 
Ø  Imependekezwa ipatikane haraka Boza, Greda na Compactor  kushindilia njia zote  zilizokwisha fanyika usambazaji wa Moram.
Ø  Secretariet itawasiliana na  Wahandisi Ben na Njau walioko KV ili kutathmin hali ya njia na maeneo  ya ndani watakayohitaji Culverts  na ushauri mwingine wowote ili kuimarisha kazi iliyokwishafanyika.
.
5.       Barabara za Vitongoji – Periphery Roads
Ø  Ufafanuzi ulitolewa kuwa barabara zinazojengwa na Lekidea ni zile zilizoainishwa katika mradi mkuu ambazo zinaunganisha vijiji vyote vya eneo hilo. Pia zile zinazokwenda kwenye vyama vya ushirika vya msingi na mashule.
Ø  Barabara ndogo ziingiazo ndani ya vitongoji, zimewekwa kama ‘Peripheral  roads’ za Lekidea ambazo LEKIDEA haitaweza kufanyia kazi katika mradi huu mkuu bali familia zinazotumia barabara hizo ndogo zikipenda  watachanga kwa ajili ya ukarabati wa njia hizo specific na LEKIDEA inaweza kusaidia usimamizi zikatengenezwa ipasavyo. Hivyo ieleweke kuwa  barabara  ndogo ndani ya vijiji au vitongoji, watachangia  wahusika watumiaji wa njia hizo na LEKIDEA inaweza kusimamia kazi husika.

6.       Uzinduzi Rasmi
Ø  Lilitolewa pendekezo kuwa aombwe Kiongozi fulani afungue barabara zetu. Wazo hili lilikubalika kwa kiasi ila litahitaji kupata maoni ya wajumbe wengine.
Ø  Kutokana na shughuli hii ya Uzinduzi kuwa muhimu sana, ilipendekezwa Ndg Venance Msaki pamoja na Savinus Kessy watasaidia kuonana na Ndg Dennis Msacky (wa Mwananchi) ili awezeshe kumwona Mgeni aliyependekezwa pindi tutakapo kubaliana katika hatua hii. Mgeni rasmi huyo wa ufunguzi atakuwa muhimu kwetu katika suala zima la Fund-Raising kwa ajili ya miradi inayoendelea ambayo ni ya kufufua zao la Kahawa na kupanda miti na Mazingira.
Ø  Pia pendekezo la kumtumia Ndg Dennis Msacky kuweka Makala ya Miradi na majukumu ya LEKIDEA katika gazeti la Mwananchi aliachiwa V. Msaki alifuatilie.
  
7.       Michango.

Ø  Martin alitoa taarifa fupi  ya michango ambayo  imeshaelezwa juu  ni mil.24. Ukipunguza deni la trip 100 ambazo ni sh.12,000,000, baki ni 12,000,000. Michango zaidi inatakiwa kuwezesha Moram kuendelea.

Ø  Taarifa ya Makusanyo na Matumizi hadi siku ya Kikao
Taarifa kama ilivyowasilishwa na Ndg Emilian Saluo ilikuwa kama ifuatavyo:
·         Makusanyo Jumla ni Sh 65,866,626/-
·         Kiasi cha hela haijaja  ni 26,746,000.
·         Jumla ya matumizi ni 42,860,410
·         Balance kufikia leo  24,100,000

Kiasi kinachokuwa bado kinadaiwa toka kwa wachangiaji  ni 26,746,000 ambayo inatoka  kwa waliokwisha ahidi, fedha ambayo inahitajika kukusanywa mapema sana ili kumaliza kazi iliyosalia. Ilionekana kuwa hawa walioahidi na bado kutoa fedha wanakwamisha malengo yetu. Imekubalika kwa majina yote yachujwe  yatangazwe kwa jamii yetu. Iliafikiwa kuwa majina  hayo yawasilishwe kwa Bw  Njau ili awasilishe  kwa Paroko ayatangaze kanisani  ili jamii iwatambue wagumu hao.
 
8.        Mengineyo.

Ø  Michango iendelee kuhamasishwa kwa SMS , hii iliafikiwa kuwa iwepo  njia ya kutuma SMS  kwa kila mdau. Uwepo muda fulan ambapo kikao kikiafiki fedha kiasi  zitatoka kulipia central-SMS ambayo atatumia Paul Msaki  kusambaza SMS kwa mtandao, Secretariet  itajadili.
Ø  Pia ilipendekezwa kuwa sms fupi  na nzuri iandaliwe  itumwe kwa wote hasa wale ambao  wanagoma, ili angalau watoe kiasi chochote na kila apataye SMS hiyo aisambaze pia kwa wengine .

Kikao kilifungwa saa 3:15 usiku kwa sala

Waliohudhuria-
1.       Edward Msaky – M/Kiti - LEKIDEA
2.       Joseph Shewiyo – Katibu -
3.       Martin M Kessy
4.       Paul Msaki
5.       Thomas Msaki
6.       Savinus Kessy
7.       Venance V Msaki



--------------------------------------            --------------------------------------
Katibu                                                    M/Kiti
LEKIDEA


---------------------------------------------------------------------

 ZIFUATAZO NI  BAADHI TU YA PICHA ZA MATUKIO YA UJENZI KATIKA MAENEO MBALIMBALI YA BARABARA ZETU ZA LEGHO-KIRUA VUNJO MASHARIKI, MRADI UNAOSIMAMIWA NA TAASISI YETU YA LEKIDEA.

---------------------------------------------------------------------

Kwa dhamira moja, kazi ya kuchonga Barabara zote muhimu kama zilivyoainishwa katika 'Mradi Mama' wa LEKIDEA zilianza kwa kasi kubwa pasipo kizuizi chochote kikubwa, na kulingana na malengo na matarajia, kazi ya uchongaji ilikamika vyema kama inavyoonekana pichani juu, hii ikiwa ni sehemu ya barabara ielekeayo Kisanja-Legho KV.
Hii ni sehemu muhimu ya Makutano ya 'Kitaarinyi' katika Barabara ya kutoka Kisomachi hadi KNCU au Mero Kati. Barabara imefanyiwa kazi bora, na hapa inaonekana Greda lilisambaza Moram na kusawazisha vyema.
Baada ya Kazi kubwa ya Greda kuchimba, kusawazisha na kusambaza Moram uliomwangwa katika barabara zetu, kazi muhimu ni ya kushindili. Hapa linaonekana 'Shindilia' likifanya kazi yake na kuimarisha zaidi dhidi ya mmomonyoko.


Maeneo mengine mengi kazi zimefanyika kwa kujitolea na kwa kiwango bora sana. Hapa inaonekana Greda likisambaza Moram na kuweka mikondo ya kuelekeza maji ya mvua pembeni ili yasiharibu barabara. Vijana wetu wanaonekana wakipita kwa hamasa wakishuhudia kazi iliyokuwa inaendelea
Kazi ya nguvu inaendelea, kusambaza na kusawazisha Moram. Pamoja na kazi ikiendelea, wananchi walikuwa wakiendelea kufaidika na huduma hii muhimu ya barabara kwa walio na usafiri binafsi na pia mama zetu waendao mashambani, sokoni na maeneo mengine ya huduma za jamii. Hakika maendelea yanakuja vyema.


KAZI ZAIDI ZINAENDELEA,  UWEKAJI NA USAMBAZAJI WA MORAM KATIKA NJIA ZOTE MUHIMU, IKIWA NI PAMOJA NA KUKARABATI MAENEO KOROFI ENDAPO MVUA ZITALETA HITILAFU YOYOTE, HAYA YOTE TATAFANYIKA VYEMA.

KADHALIKA, NJIA ZA VITONGOJI PIA ZIMEPEWA KIPAUMBELE HASA KWA MICHANGO YA WAZALIWA WA MAENEO HUSIKA (AU FAMILIA) AMBAPO NJIA HIZO ZINAPITA. WANAWEZA KUJIUNGA NA KUCHANGIA KWA PAMOJA KUIMARISHA MAENEO YAO. WACHANGIAJI WANAWEZA KUCHANGA NA KUELEKEZA KUWA 'MCHANGO WANGU/WETU WA GREDA/MORAM AWAMU HII UKAFANYIE KAZI KATIKA NJIA AU MTAA/KITONGOJINI KWETU'...LEKIDEA IPO TAYARI NA ITAJITAHIDI KUTIMIZA HILO KULINGANA NA UMOJA WA WAHUSIKA NA HALI HALISI NA KIWANGO CHA WACHANGIAJI HAO ILI KUTOKUSABABISHA TATIZO.
TUCHANGAMKE, MUDA NDIO SASA, KUJENGA ASILI YETU.

PAMOJA TUTAFIKA NA KUFANIKIWA. TUUNGANISHE NGUVU!
TUCHANGIE BILA KUKATA TAMAA, NI MAENDELEO YETU WENYEWE.

---------------------
Michango ya LEKIDEA inaweza kuwasilishwa kwa CASH au kwa njia zifuatazo.
CRDB A/C: 0152095786500; 
LEGHO KIRUA DEVELOPMENT ASSOCIATION
Kwa Simu: Vodacom MPESA– 0755 799 133; TigoPESA- 0653 799 133

Muda ndio sasa, TUCHANGIE, TUENDELEE MBELE!!.

TYK...
Secretariat - LEKIDEA