IFUATAYO NI TAARIFA FUPI YA KIKAO CHA TATHMINI YA MIRADI, 2012, NA DIRA MPYA 2013.
-------------------------
-------------------------
KIKAO CHA LEKIDEA
KUTATHMINI MIRADI YA LEKIDEA
NA DIRA YA MWAKA MPYA 2013
Venue: DOUBLE VIEW HOTEL, SINZA – DSM.
Date: 02/12/2012
MINUTES ZA KIKAO
AGENDA
|
1. Writeups: Food Aid
& JICA nk.
2. Media Conference na
Statement kwa Wana-LEKIDEA na Umma wote.
3. Programme na Dira ya
Mwaka Mpya 2013.
4. Ada ya Kila
Mwana-LEKIDEA na Manufaa yake.
5. Mengineyo
|
MCHANGANUO WA AGENDA
|
Kufungua Kikao:
Kikao
kilifunguliwa saa 12:00 jioni kwa sala.
1.
Writeups: Food Aid & JICA:
Ø
Kikao
kiliafikiana kuwa Katibu, Ndg Joseph Shewiyo ataandaa Draft ya Writeups na
kuiwasilisha kwa Sekretariat ambayo itaipitia, kuijadili na kuikamilisha
mapema kwa ajili ya kusambaza ktk taasisi mbalimbali ikiwa ni pamoja na Food
Aid na JICA ili kutafuta ufadhili wao kwa miradi ijayo ya LEKIDEA.
2.
Report ya Sekretariat kwa Wana-LEKIDEA
na Umma
Ø
Sekretariat
iliwasilisha taarifa kwa ufupi kuhusu mradi wa barabara ulivyokwisha kufikia
hadi sasa, na malengo yajayo ili kuhakikisha kuwa tuna maendeleo endelevu.
Ø
Kikao
kiliafiki kuwa iandaliwe Taarifa rasmi (Media Statement) ya jumla,
itakayounganisha ile Taarifa kwa Umma iliyotoka awali pamoja na Taarifa mpya
ya mwaka mpya itakayotoka hivi karibuni, ili iwasilishwe kwa vyombo vya
Habari katika mipangilio ifuatayo:
ü
Katibu
kuandaa makala ili itolewe kwenye vyombo vya habari.
ü
Iandaliwe
Taarifa iliyokamilika vyema (Media Statement), ikionyesha Profile ya LEKIDEA
na miradi yake na mafanikio hadi sasa.
ü
Taarifa
hii pia itaunganisha taarifa ya awali iliyotolewa kwa Vyombo vya Habari,
pamoja na taarifa mpya ya Mwaka Mpya 2013, pamoja na picha za wananchi na
Miradi ilivyokuwa inafanywa, na Video za kazi zilivyokuwa zikiendelea.
ü
Mh
Diwani Alex Umbella aliahidi kuwasilisha video za matukio hayo ili ziweze
kutumika ktk kuandaa Media Conference hiyo.
ü
Tukio
hili litawasilishwa na M/Kiti, pamoja na Katibu au Kaimu Katibu, ktk Ukumbi
wa HABARI MAELEZO, na maandalizi yanafanyika ili iweze kufanyika kabla ya
Tarehe 15/12/2012.
3.
Programme Kubwa na Dira ya Mwaka Mpya
2013:
Ø
Kikao
kiliafiki kuwa katika kuendeleza malengo ya mafanikio ya wananchi wetu,
LEKIDEA imeainisha malengo na mipango kabambe kwa Mwaka Mpya 2013 kama
ifuatavyo:
ü
Kumalizia
ujenzi wa barabara kwa kujenga culverts na barabara ndogondogo za ndani, pia
kuongezea moram sehemu zenye upungufu
ü
Kuanzisha vitalu vya miche ya miti
hususan ya Mierezi
(gravelia) ipatayo 10,000/- (elfu kumi) kwa kuanzia ambayo itatolewa kwa
wanavijiji ili wapande katika maeneo mbalimbali ya ukanda wetu ikijumuisha
kando ya barabara zetu, na ktk kingo za mashamba.
ü
Mhe Diwani atafuatilia ufufuaji na
uendelezaji wa bwawa la Urenga kwa kuhimiza Halmashauri ya Wilaya ilifufue na kuliendeleza kwa ajili
ya umwagiliaji. Hili litawezesha
wananchi wetu kufaidika na Samaki, na umwagiliaji wa Mboga na mazao
mengineyo.
ü
Harambee ya kuchangisha hela za
maendeleo ya miradi ya Lekidea kufanyika ndani ya Februari 2013 ili kuwahi
mvua za Masika kwa ajili ya Moram, Maintenance ya Njia na Coverts nk.
4.
Ada ya Kila Mwana-LEKIDEA
Ø
Kikao
kiliafiki kuwa ili kuwezesha taasisi yetu iweze kusonga mbele kwa mafanikio
na kuwatumikia wananchi pasipo kukwama popote, kila mwana-LEKIDEA na
mpenda-maendeleo atatoa ada ya kudumu ya Sh
100,000/- (Laki moja) kwa mwaka,
ada ambayo itakuwa nyezo kwa LEKIDEA na Malengo yake ya muda mrefu
LEGHO-KIRUA ikiwa ni pamoja na utekelezaji wa yafuatayo:-
ü
Lengo kuu; Kuendeleza, Kusimamia
(Maitenance) Barabara
zetu zote kwa kipindi chote cha mwaka mzima.
ü
Lengo jingine; Ada hii pia itatumika kama sehemu ya
uchangiaji wa masuala ya maendeleo endelevu ya Legho-Kirua na hivyo LEKIDEA
itatambua na kuthamini sana nafasi na kipaumbele cha mchangiaji katika
kushirikiana naye masuala ya kijamii.
ü
Manufaa kwa Mtoa Ada: Kutokana na umuhimu wa kuwezesha
maendeleo yetu kuwa endelevu, LEKIDEA itamtambua na kumthamini kila mtoa ada
ya uanachama kwa kuhamasisha wengine kushirikiana naye katika masuala muhimu
ya kijamii atakayokabiliana ikiwa ni pamoja na matukio kama Misiba, Harusi, Magonjwa nk.
ü
Madhara ya Kutokutoa ada; Wapo wazaliwa wa Legho-Kirua ambao
mbali na kusikia, kuhamasishwa na kusukumwa sana kuchangia maendeleo na
miradi yetu, wamekuwa wagumu sana, wengine wakibeza, na kudharau juhudi hizi,
na pia wengine kuwakwaza wengine ili tu kuwakatisha tamaa wasichangie umoja
huu. Huu ni mwenendo usiokubalika.
ü
Hivyo
basi, kulingana na umuhimu wa ada hii kwa maendeleo ya jamii yetu, mwananchi
atakayekwamisha au kushindwa kuunga mkono na kutoa ada hii kwa malengo yasiyo
dhahiri, au kwa visingizio visivyoeleweka, wakati ukweli ni kuwa,
ameshafaidika na anafaidika kwa sasa na ataendelea kufaidika na jasho la
wengine wapenda maendeleo wa Legho-Kirua waliokwisha kuchangia kwa hali na
mali, taasisi ya LEKIDEA haitamvumilia mtu wa mwenendo huo, na haitasita
kumfichua, na pia kuwafahamisha wanachama na wananchi wote wapenda maendeleo
wa Legho-Kirua ili watambue mwenendo wa mtu husika, na hata ikiwezekana,
LEKIDEA itachukua jukumu la kwanza kuhamasisha pale inapowezekana ili
mwananchi kama huyo asiweze kuungwa mkono, au kuchangiwa katika masuala ya
kijamii kama misiba, harusi, magonjwa nk. ‘Asiyeotesha nawe hawezi kuvuna nawe’
5.
Mengineyo
Ø
Lobbying: Kikao kilipendekeza uwepo mpango wa
kukutana na Engineer wa Manispaa kwa Mazungumzo ya Maendeleo yetu, hasa
kuhusu budgets allocation, hasa ktk mifereji ya maji ambayo ni kati ya chaguo
letu kubwa ktk maeneo ya utekelezaji.
Kikao kilifungwa saa 3:45 usiku kwa
sala.
HAHUDHURIO:
1. Eng Simon T Njau - Makamu/MKti
2. Joseph I Shewiyo - Katibu
3. Martin M Kessy - Makamu/Katibu
4. Mh Alex Umbella - Diwani wetu
5. Emilia J Saluo - Mwanasekretariat
6. Paul Z Msaki - Mwanasekretariat
7. Stephen Vendelin Msacky - Mjumbe
8. Dr Kessy, Mkoloni - Mjumbe
UDHURU:
1. Edward F Msaky - M/Kiti
2. Eng Bernard D. Ndepachio -
Mwanasekretariat.
3. Aman Beda Kyara
4. Venance Vendelin Msacky
-------------------- ----------------------
Katibu M/Kiti
|
Katika
kuwakumbusha Wana-LEKIDEA katika kutoa michango yao, wasisite kutumia njia
zifuatazo:
|
AKAUNTI YA
LEKIDEA: Bank: CRDB BANK Plc.:
Jina la A/C: LEGHO KIRUA DEVELOPMENT ASSOCIATION
A/C No: 0152095786500
|
SIMU MKONONI
ZA LEKIDEA:
§ Vodacom – MPESA:
0755 799 133
§ Tigo – TigoPESA: 0653 799 133
|
MWISHO
|
-------------------------&&&&&---------------------------
HABARI ZA MAENDELEO YA KIRUA VUNJO MASHARIKI CHINI YA USIMAMIZI WA LEKIDEA KAMA ZILIVYORIPOTIWA NA MAGAZETI YA THE GUARDIAN NA NIASHE HIVI KARIBUNI.
---------------------------
UJUMBE NA SALAMU RASMI ZA MWENYEKITI WA LEKIDEA KWA AJILI YA X-MASS 2012 NA MWAKA MPYA 2013 KWA WATU WOTE