LEKIDEA FOCUS OVERVIEW

LEKIDEA
is a registered Non-profit Organization of Kirua Vunjo East Moshi, by Natives from related Villages (Kileuo, Mrumeni, Kotule, Mero, Legho, Lasso, Kwa-Laria(Kanji), dedicated to join together, leverage their Vision, Objectives, Social strengths, ambitions & professionalism and other common resources from members, relatives and families having any origination with K.V East, to come TOGETHER, DEVELOP and CHANGE their Motherland through Projects and involvements in different Social development Initiatives that play roles in alleviating poverty and enhancing opportunities in collaboration with all well wishers, and support from social development entities from the village level, national level, and international level.

LEKIDEA :: Tangazo la Tender - Barabara Uchira - Kisomachi

Wana-LEKIDEA, Lifuatalo ni Tangazo la Tender ya Ujenzi wa Barabara yetu ya Uchira hadi Kisomachi, kama lilivyotolewa na Manispaa ya Halmashauri na kuchapishwa katika Gazeti la Mwananchi kama linavyoonyeshwa. 


LEKIDEA KWA KUFUATILIA KWA UKARIBU MAENDELEO YOTE NA KUHAKIKISHA KUWA MPANGO HUU UNATEKELEZWA KWA UWAZI NA KWA UIMARA ILI KUFANYA BARABARA YETU IWE IMARA NA YA KUDUMU. 

TUNAWAOMBA WANA-LEKIDEA WOTE WENYE MAKAMPUNI YA UJENZI YALIKWISHASAJILIWA NA BODI YA USAJILI WA MAKANDARASI, WAWE WA KWANZA KUTUMA MAOMBI YAO MAPEMA IWEZAKANAVYO, WAKIZINGATIA VIGEZO NA MASHARTI YALIYOAINISHWA CHINI YA TANGAZO LENYEWE.
KATIKA TANGAZO HILO, MAMBO YAFUATAYO YAMEONEKANA KUTUGUSA NA PIA YATAFUATILIWA KUJUA HASA UNDANI WAKE KATIKA UTEKELEZAJI PALE MKANDARASI ATAKAPOPATIKANA:
  • LOT 5 na LOT 8 kwa pamoja zimeainisha kuhusisha Ukarabati wa Barabara yetu ya Uchira - Kisomachi - Jambo hili litafuatiliwa kuona kama kuna double-allocation ya funds au vinginevyo ili kuhakikisha kila kilichopangwa kinatumika vyema ipasavyo.
  • LOT 6, ina kipengele cha Ukarabati wa Barabara ya PAKULA hadi KILEMA. Katika Mradi wa LEKIDEA kusimamia ukarabati wa Barabara za Vijiji na Vitongoji, eneo la kuanzaia Kanji -kwa Laria hadi Lasso - Juu (Darajani), ni maeneo ya Ukanda wa LEKIDEA pia. Hivyo uongozi wa Diwani wetu hakika utaombwa kufuatilia ashirikiane na wanaohusika kusimamia kipande hiki kwani ni muhimu sana katika kuunganisha wananchi wote wa Mero, Kwa-Laria (Kanji), Lasso Kati na Lasso-Juu kwenda Kilema Sokoni (Lyamombi), Marangu Mtoni na Soko la Mwika. Barabara hii ni rahisi sana kwa wananchi hawa na ni fupi kwao pia. Hata usafiri utakuwa rahisi sana.
  • Katika Tangazo hilo, Ili kuwezesha Wana-LEKIDEA kufuatilia na kujionea yale maeneo muhimu yanayotuhusu Ukanda wetu kwa ukaribu, nimezungushia rangi wa chungwa/njano majedwali yanayohusika.



No comments: