LEKIDEA FOCUS OVERVIEW

LEKIDEA
is a registered Non-profit Organization of Kirua Vunjo East Moshi, by Natives from related Villages (Kileuo, Mrumeni, Kotule, Mero, Legho, Lasso, Kwa-Laria(Kanji), dedicated to join together, leverage their Vision, Objectives, Social strengths, ambitions & professionalism and other common resources from members, relatives and families having any origination with K.V East, to come TOGETHER, DEVELOP and CHANGE their Motherland through Projects and involvements in different Social development Initiatives that play roles in alleviating poverty and enhancing opportunities in collaboration with all well wishers, and support from social development entities from the village level, national level, and international level.

LEKIDEA :: Kilimo na Ufugaji wa Kisasa


KILIMO:

LEKIDEA IMEWEKA MIKAKATI MBALIMBALI KATIKA KUHAKIKISHA KUWA KILIMO CHA NA UZALISHAJI WA WANANCHI WANAOISHI UKANDA WETU WOTE WA KIRUA-VUNJO MASHARIKI, ILI KUKUZA KILIMO BORA, CHA UTAALAMU, ILI KUZALISHA BIDHAA BORA, NA ZENYE KUUZIKA, IKIWA NI PAMOJA NA NDIZI BORA, MATUNDA, KAHAWA, MBOGAMBOGA, MAZIWA; NK.

Miche ya Ndizi yafaa kustawishwa vyema ili izae vyema
Ndizi iliyostawishwa vyema huzaa ndizi bora kwa chaluka na biashara

Ustawi unaoonyesha Mafanikio, mikungu miwili au zaidi katika kitalu kimoja
Ndizi kubwa mfano huu ni kutokana na matunzo mema na hivyo kuzidisha uzalishaji kwa ajili ya chakula na biashara, na ufanisi kama huu unawezekana kwa Wananachi wa Ukanda wetu.

Pia Ndizi ikeshavunwa, ni vyema kuchambuliwa na kuhifadhiwa vyema ndani ya Maji safi kwa ajili ya kula au kusafirisha kwa biashara.
Ndizi zikeshazalishwa kwa wingi hufanya Wananchi kuneemeka kwa Biashara na kusafirishwa ndani na nje ya Ukanda wetu na hasa kama Huduma ya Barabara ni nzuri na ya kuaminika. Barabara ni muhimu sana kwa wananchi wetu.
  
Kilimo Bora Cha Mahindi huwezesha Uzalishaji na Mavuno kuwa Bora
Dalili za Mavuno Bora ya Mahindi kwa wananchi wetu hujionyesha mapema
Mahindi yaliyotunzwa kwa Ubora hukomaa vyema na kuwezesha Chakula kiwe cha auhakika.

Mahindi yaliyolimwa kwa ubora, hukomaa na kukauka vyema, na kuwa tayari kuhifadhiwa, au ziada kuwasilishwa masokoni kwa ajili ya biashara, na hii huzidisha kipato cha wananchi na kufuta umaskini.
 
KAHAWA pia ikitunzwa vyema huzaa vyema kwa Manufaa ya Wananchi wetu.

KAHAWA iliyozaa vyema tayari kwa kuchumwa
----------------------&&&---------------------------
KILIMO CHA MBOGAMBOGA


LEKIDEA inasisitiza Uzalishaji mwingi wa Mbogamboga ambao huwajengea wananchi uwezo wa kimaisha na kibiashara katika kujikwamua na kuondokana na Umaskini.
Kilimo cha Mbogamboga chaweza kusitawishwa vyema pia katika ukanda wetu wote kwa ajili ya wananchi wetu na hata kwa biashara.
Mashamba na Bustani Bora za Mboga - Kabeji, kama inavyoonekana juu, itanufaisha wananchi wetu kwa chakula na biashara.
Bustani za Nyanya zilizostawishwa vyema ni dalili ya mavuno mema.
Nyaya iliyozaa vyema inakomaa vyema, na hunufaisha Mkulima.
Nyanya iliyostawi na kukomaa vyema huwa na Mavuno bora ambayo hukuza kipato cha mwananchi/mkulima.
Uzalishaji mwingi wa Mbogamboga Kwa Biashara huwajengea wananchi wetu uwezo wa kimarika kibiashara katika kujikwamua na kuondokana na Umaskini.

----------------------------&&&&&----------------------

 UFUGAJI WA KISASA:

 ----------------------------&&&&&----------------------

Ufugaji wa Kuku wa Kisasa utasaidia Wananchi wetu kimahitaji.
LEKIDEA inalenga kuhamasisha na kukuza ufugaji wa Kuku wa Kisasa kwa Wananchi wetu

Ufugaji wa Mbuzi yafaa uwe wa Kisasa zaidi

Ufugaji wa Mbuzi wa Kisasa

Mbuzi wa Kisasa huzaa kwa Manufaa na pia hufanikisha kukua kwa idadi ya mifugo.

LEKIDEA ina malengo ya kuhamasisha Wananchi wa Ukanda wetu Kufuga Mbuzi wa Kisasa kwa ajili ya Nyama na Maziwa kama wanaoonekana na inapowezekana waweze kupatiwa misaada ya huduma za Tiba ya mifugo na ukaguzi.

Uugaji wa Nguruwe unanufaisha Wananchi kibiashara.
Matunzo ya Nguruwe haka hivi, hasa kwa maeneo ya Vijijini kwetu ni wa muhimu na unatekelezeka endapo wananchi watahamasishwa na kuwezeshwa ipasavyo.

Nguruwe wakitunzwa vyema huzaliana haraka na hivyo kukuza kipato cha wananachi. Lengo la LEKIDEA ni kufanya mafanikio kama haya yaweze kutekelezeka kwa manufaa ya Wananchi wetu vijijini.
 
Ufugaji wa Ngombe wa Kisasa pia utawasaidia sana wanaviji wetu kujikwamua kiuchumi

Wananchi wetu wanaweza kuwezeshwa katika mikopo ili waweze kuimarisha ufugaji wa Ngombe kama hawa kwa ajili ya Maziwa, Nyama na Mbolea, na hivyo kukuza kipato na maendeleo yao na kufuta kabisa umaskini.

 NI LENGO LA LEKIDEA KUHARAKISHA MAENDELEO KATIKA NYANJA ZOTE HIZI IKISHIRIKIANA NA TAASISI ZOTE MUHIMU ZA KIKANDA, KITAIFA NA HATA KIMATAIFA ILI KUINUA MAISHA, USTAWI NA MAENDELEO YA WANANCHI WA UKANDA WETU WA KIRUA VUNJO MASHARIKI.

TUSHIRIKIANE WOTE, TUCHANGIE, TUJENGE NGUVU MOJA TUENDELEZE NYUMBANI KWETU, TUBADILI HISTORIA YA UMASKINI WA WANANCHI WETU.

5 comments:

Anonymous said...

hongereni na mungu awatie nguvu msikate tamaa

Anonymous said...

Kwa kweli mnastahili pongezi hongereni sana.

Zacharia Lema said...

Jamani huu ndio mfano tunaohitaji kuiga ili kufanikiwa kuondokana na umasikini.
Mbarikiwe sana.

Anonymous said...

Good work LEKIDEA.
How can you reached for more training and learning?

Unknown said...

Nahitaji kufanya Mahojiano na MKULIMA aliyefanikiwa kwa Kutueleza Changamoto na Nini alikifanya mpaka kufikia Malengo yake Na PIA ni nafasi ya mkulima kujitangaza kwa biahsara yake anayoifanya,,, HII NI tv pROGRAM kWA ALIYE tAYAR, kUFANYA mAHOJIANO NAMI Anitafute +255 653 32 44 07