LEKIDEA FOCUS OVERVIEW

LEKIDEA
is a registered Non-profit Organization of Kirua Vunjo East Moshi, by Natives from related Villages (Kileuo, Mrumeni, Kotule, Mero, Legho, Lasso, Kwa-Laria(Kanji), dedicated to join together, leverage their Vision, Objectives, Social strengths, ambitions & professionalism and other common resources from members, relatives and families having any origination with K.V East, to come TOGETHER, DEVELOP and CHANGE their Motherland through Projects and involvements in different Social development Initiatives that play roles in alleviating poverty and enhancing opportunities in collaboration with all well wishers, and support from social development entities from the village level, national level, and international level.

Sunday, March 22, 2015

LEKIDEA: UFUNGUZI WA OFISI: BAADHI YA PICHA ZA TUKIO LA UFUNGUZI WA OFISI, JUMAMOSI 21/03/2015

WADAU

​ WANA-KV MASHARIKI​ (LEKIDEA)


SIKU YA JANA JUMAMOSI, ILIFUNGUA UKURASA MPYA. MWENYEKITI WETU NDG EDWARD FABIAN MSAKY ALIMKABIDHI RASMI OFISI KARANI WA LEKIDEA [STELLA NJAU] ILI KUANZA MAJUKUMU KESHO.

OFISI HIZO ZIPO GHOROFA YA 4, NDANI YA JENGO LA S & F HOUSE, JENGO LIPO MWANANYAMALA, [KOMA-KOMA], AMBALO KWA CHINI IPO BANKI YA AKIBA COMMERCIAL. JENGO HILO LINALOMILIKIWA NA MWANA-LEKIDEA, ENG. SIMON TEOBALD NJAU.

MUNGU AMEIJALIA SANA KV KUWA NA WATU WENYE MOYO WA KUJITOLEA, NA WENYE VIPAJI MBALIMBALI, NA WANABARIKIWA ZAIDI KWA JINSI WANAVYOJITOLEA.
ZIFUATAZO NI KATI PICHA ZA TUKIO HILO MUHIMU, PICHA ZINAANZIA NA JENGO LENYEWE, IKIFUATIWA NA MATUKIO A KUFUNGUA VIFAA NA KUUNGANISHA VIFAA HIVYO [COMPUTERS], KAZI ILIYOFANYWA NA KATIBU WA SECRETARIAT YA LEKIDEA [PAUL SANENE MSAKI].

PICHA NYINGINE ZATATUMWA PIA KTK MTANDAO Facebook, ktk KURASA WA LEKIDEA; Unatakiwa tu kutafuta [seach] Legho Kirua Development Association., utakutana na picha link ya picha hizo

TUFUATILIE, TUCHANGIE TUSONGE MBELE!!

PAMOJA TUSONGE MBELE!
PAUL MSAKI
Katibu wa Sekretariat - LEKIDEA.

--------------------------------------------------------------------
Jengo la S & F likionekana kwa nje



Mlango wa Kuingia ktk Ofisi za LEKIDEA, ghorofa ya 4



M/Kiti na Karani wa LEKIDEA wakiwa wamesimama pamoja na Vifaa ndani ya Ofisi ya LEKIDEA


M/Kiti wa LEKIDEA [Edward Msaki] pamoja na Katibu wa Secretariat [Paul Msaki], kwa pamoja wakifungua Vifaa vya Ofisi [Computer], wakati huo Karani wa LEKIDEA [Stella Njau] akiangalia tayari kupokea majukumu.






M/Kiti kimwelekeza Karani baadhi ya masuala ya Majukumu yake ikiwa ndio kukamilisha Makabidhiano kamili ya Offisi na Vifaa.



Ofisi ya LEKIDEA inavyoonekana kwa nje! Ni Ofisi ya Kisasa kabisa yenye A/C [vipooza hewa]

Katibu wa Secretariat ya LEKIDEA, ambaye pia ni Mtaalam wa Technolojia ya Mawasiliano [IT] akiunganisha Vifaa vya Ofisi tayari kwa kutumika.



Katibu wa Secretariat akijaribu Computer baada ya kukamilisha ufungaji wake na hivyo kuwa tayari kwa Karani kuanza kazi rasmi.

Karani wa LEKIDEA Stella Njau akikalia usukani wa Ofisi yake tayari kwa kuanza kutekeleza kazi za maendeleo ya LEKIDEA

WOTE TUUNGE MKONO, TUSHIRIKIANE TUFANIKISHE MAENDLEO YA UKANDA WOTE WA KIRUA VUNJO MASHARIKI IKIJUMUISHA MAENEO YOTE YA LEGHO, MULLO, LASSO, MERO, KILEUO, MRUMENI HADI UKANDA WA NGANJONI.

KARANI WA LEKIDEA ATAFANYA KAZI ZAKE KILA SIKU KUHAKIKISHA KUWA MAWASILIANO YANAWAFIKIA, NA MCHANGO WA KILA MMOJA WETU UNATAMBULIWA NA KUHESHIMIKA KATIKA KUCHANGIA MAENEO YA URITHI WETU PALE TULIPOZALIWA, YAANI KIRUA VUNJO MASHARIKI, INAYOSIMAMIWA NA TAASISI YETU RASMI YA Legho Kirua Development Association (LEKIDEA), iliyosajiliwa rasmi tangu 2008!

PAMOJA DAIMA TUTAFANIKIWA ZAIDI.

Tuesday, March 10, 2015

LEKIDEA: MANUNUZI YA LAMI PIPA 300 YAKAMILIKA - 07/03/2015

ZIFUATAZO NI BAADHI  YA PICHA KATIKA HATUA MBALIMBALI ZA MAANDALIZI YA UNUNUZI WA LAMI. IKIFUATIWA NA MANUNUZI, UPAKIAJI- JIJINI DAR ES SALAAM (TOKA KAMPUNI YA SIBIKA TRADERS/COMMODITY GROUP LTD) TAREHE 07/03/15 USAFIRISHAJI NA USHUSHAJI WA MAPIPA 300 YA LAMI YA LEKIDEA-UCHIRA SEKONDARI 08/03/15.
Kikao cha Uongozi wa LEKIDEA kilichokaa tarehe 19/02/2015 na kutoa maamuzi ya kukamilisha ununuzi wa Mapipa 300 ya Lami kwa ajili ya Mradi wa kampeni ya 'Tokomeza Mawe kwa Lami, pale Mawonyi' iliyolenga uwekaji lami kipande cha zaidi ya 2km katika Barabara ya Uchira-Kisomachi-KwaLaria
Sehemu ya Mapipa 300 ya LEKIDEA yakiwa ktk Yadi ya Kampuni ya Sibika/Commodity Group Ltd tayari kwa kupakiwa ktk malori kusafirishwa kwenda Uchira Sekondari.



Sehemu ya Mapipa 300 ya LEKIDEA yakiwa ktk Yadi ya Kampuni ya Sibika/Commodity Group Ltd tayari kwa kupakiwa ktk malori kusafirishwa kwenda Uchira Sekondari

Sehemu ya Mapipa 300 ya LEKIDEA yakiwa ktk Yadi ya Kampuni ya Sibika/Commodity Group Ltd yakiwa yanapakiwa ktk malori kusafirishwa kwenda Uchira Sekondari

Lori mojawapo kati ya Malori manne yaliyokwishapakiwa mapipa ya lami, likwa tayari kuanza safari kuelekea Uchira - Moshi, tarehe 07/03/2015

Lori mojawapo likiwa tayari limewasili Uchira, katika barabara ya Uchira-Kisomachi kuelekea Uchira Sekondari kupakua lami.

Lori la pili likiingia barabara ya Uchira - Kisomachi kuelekea Uchira Sekondari kupakua lami

Vijana wa KV wakichangamka kushusha Mapipa ya Lami eneo la Uchira Sekondari ili kuyapanga eneo lililotengwa.

Vijana wa KV wakichangamka kushusha Mapipa ya Lami eneo la Uchira Sekondari ili kuyapanga eneo lililotengwa.

Vijana wa KV wakichangamka kushusha Mapipa ya Lami eneo la Uchira Sekondari ili kuyapanga eneo lililotengwa.

Vijana wa KV wakichangamka kushusha Mapipa ya Lami eneo la Uchira Sekondari ili kuyapanga eneo lililotengwa. Na kushoto ni Diwani wa Kata ya Kirua Vunjo Mashariki, Mh Alex Umbella akisimamia upakuaji wa mapipa ya Lami .

Vijana wa KV wakichangamka kushusha Mapipa ya Lami eneo la Uchira Sekondari ili kuyapanga eneo lililotengwa.

Vijana wa KV baada ya kushusha Mapipa ya Lami eneo la Uchira Sekondari wanaendelea kuyapanga eneo lililotengwa.


Vijana wa KV wakichangamka kushusha Mapipa ya Lami eneo la Uchira Sekondari ili kuyapanga eneo lililotengwa.

Vijana wa KV wakichangamka kushusha Mapipa ya Lami eneo la Uchira Sekondari ili kuyapanga eneo lililotengwa.

PICHA ZA MATUKIO YA UJENZI UTAKAPOANZA ZITAWASILISHWA HAPA KTK MTANDAO WETU MAPEMA IWEZEKANAVYO.

Saturday, March 7, 2015

BAADHI YA PICHA ZA UJENZI BARABARA YA UCHIRA-KISOMACHI-KWA LARIA UKIENDELEA DESEMBA 2014





Makalavati yakiwekwa eneo la barabara ya Kileuo - karibu na 'Kwa Kinyala' au kwa 'Mara-moja'

Makalavati yakiwekwa eneo la barabara ya Kileuo - karibu na 'Kwa Mwl Vitali Kessy'

Makalavati yakiwekwa eneo la barabara Mtembonyi - karibu na 'Idara ya Maji'





Barabara yetu, eneo la Msufini

Makalavati yakiwekwa eneo la barabara - karibu na 'Kwa Mtanzania'


Barabara yetu eneo la Kiorotsunyi



Barabara yetu eneo la juu ya Mawonyi - 'Kwa Lotoronge'

Makalavati yakiwekwa eneo la barabara Mawonyi 

Nyingi kati ya kazi hizi zilikamilika na nyingine zinaendelea ili kuhakikisha kiwango kinachotakiwa kimefikiwa na pia ukanda wote wa kuanzia Uchira hadi juu ya Mawonyi, umbali wa 2km panaimarishwa ipasavyo kwa ajili ya uwekaji wa Lami utakaoanza siku sio nyingi. Pamoja daima tutafanikiwa zaidi.