LEKIDEA FOCUS OVERVIEW

LEKIDEA
is a registered Non-profit Organization of Kirua Vunjo East Moshi, by Natives from related Villages (Kileuo, Mrumeni, Kotule, Mero, Legho, Lasso, Kwa-Laria(Kanji), dedicated to join together, leverage their Vision, Objectives, Social strengths, ambitions & professionalism and other common resources from members, relatives and families having any origination with K.V East, to come TOGETHER, DEVELOP and CHANGE their Motherland through Projects and involvements in different Social development Initiatives that play roles in alleviating poverty and enhancing opportunities in collaboration with all well wishers, and support from social development entities from the village level, national level, and international level.

Friday, August 23, 2013

LEKIDEA :: TAARIFA YA DIWANI, BOQs ZA BARABARA NA MPANGO MKAKATI WA KATA 2010-2020

Wapendwa Wana-LEKIDEA;

Ni fursa ya kipekee kuwa tena kukutana katika mawasiliano ya Mtandao wa Blog yetu, pamoja na kupita kitambo kidogo tangu kukamilika vyema kwa miradi yetu mbalimbali, na hasa mradi mkubwa wa Barabara za Vijiji vyetu. Ni katika kuendeleza mshikamano na hamasa zetu za kimaendeleo, hatuna budi kutokurudi nyuma katika harakati hizi ambazo ndio msingi wa heshima na kujitambua asili yetu na uzao wetu pasipo kujisahau kuwa maendeleo ni sisi wenyewe.

Ni katika kuendeleza mshikamano wetu bila kujali dini siasa, jinsia na hali ya mtu, na hata kuungwa mkono na serikali ngazi mbalimbali. Hii ni ktk kutambua juhudi zetu na hivyo kutuunga mkono katika nyanja mbalimbali za kijamii, kama inavyozidi kudhihirika katika taarifa ifuatayo. Ifuatayo ni TAARIFA TOKA KWA DIWANI wetu Ndugu ALEX UMBELLA kama inavyowasilishwa..wote tuipitie kwa umakini, . Taarifa hii pia inaambatana na BOQs za Ujenzi wa Barabara zetu (Uchira - Kisomachi, na Mabungo - Nganjoni hadi Legho) zinavyoendelea, pamoja na MPANGO MKAKATI 2010 - 2020 wa Kata yetu ya KV Mashariki.

Ni fursa kwetu wote leo hii tuone ni jinsi gani tulivyo na hazina kubwa ya kiuongozi, na viashiria vya maendeleo na mafanikio zaidi katika Kata yetu na hivyo kutokudumaa au kukata tamaa kutonana na fikra za wachache wanaovunja wengine moyo, bali tuhamasike, kuendeleza kwetu na maeneo yanayotuzunguka, tuungane zaidi na hasa katika huduma za kijamii.

Taarifa hizi pia nakala zilitumwa katika mtandao wa e-mail wa LEKIDEA. -----------------------------------------------------------------------------------------------------------------

TAARIFA YA DIWANI, BOQs ZA BARABARA 
NA MPANGO MKAKATI WA KATA KIRUA VUNJO MASHARIKI - 2010-2020
 
 
Mh. Alex J. Umbella

Wapendwa wana LEKIDEA

Napenda kuvunja ukimya na kuchukua fursa hii ya pekee kuwashukuru kwa jitihada maalum mlizozitoa kwa ajili ya maendeleo ya Legho Kirua. Jitihada zilianza na ujenzi wa Kanisa la Karmel hatimaye zikapata msisimko upya wakati wa ujenzi wa awamu ya kwanza ya miundombinu ya barabara za Vijiji. Hapana shaka tukio hili la ujenzi wa barabara lilivuta hisia nyingi toka kwa Jamii na taasisi zinazotuzunguka hasa ndani ya LEKIDEA, huku baadhi ya watu wakihoji hatma na azma tuliyojiwekea. Kwa vyovyote vile hatuna budi kumshukuru Mwenyezi Mungu kwa kutuvusha na kutuondolea hofu kwenye changamoto za kisiasa na nyinginezo zilizojitokeza na hatimaye kutupeleka kwenye Dira ya Maendeleo tuliyojiwekea.

Michango iliyoelekezwa kwenye ujenzi wa barabara takribani milioni themanini imetujengea heshima kubwa ndani ya jamii ya wanalegho na Mkoani na hasa ndani ya Halmashauri ya Wilaya ya Moshi ambako nasimamia na kutetea masilahi ya wananchi wa Kata ya Kirua Vunjo Mashariki. Ikumbukwe ujenzi wa barabara haukufanywa kwa kificho, nilikaribisha timu ya Halmashauri ya Wilaya ya Moshi hususan Mkurugenzi Mtendaji, Afisa Mipango na Mhandisi wa ujenzi kutembelea Kirua Vunjo kuona ni jinsi gani kazi ilivyokuwa ikifanyika.

Kilichowavutia na kuwashangaza ni matumizi ya mashine maalum za ujenzi wa barabara ambazo ni nadra sana kuonekana Vijijini mf. Caterpillar, bulldozer, roller, excarator. Nawashukuru sana kwa uhamasishaji uliofanywa na viongozi wa LEKIDEA kwani wananchi wenye mashamba yanayopakana na barabara walionyesha ukomavu wa hali ya juu katika kuyapokea mabadiliko.

Barabara zilizochimbwa, kuwekwa moram na kushindiliwa kwa roller zimeweza kuhimili vishindo vya mvua za masika zilizokuwa nyingi na kutikisa sehemu mbalimbali za nchi kwa sababu hiyo, barabara za Madukani – Kilasanioni, Madukani – Kisanja, Madukani – Kiwelewele (via kwa W. Matay), na Madukani – Mrumeni (kwa Mkoloni) zimeweza kupitika kipindi chote cha mvua kwa magari na pikipiki. Kadhalika kiwango cha usafi hasa wa viatu na mavazi kwa wananchi wetu kimepanda kipindi cha mvua.

Zaidi ya hayo ujenzi wa barabara uliotekelezwa na LEKIDEA umekuwa wa kiwango kikubwa zaidi kuliko ujenzi ulifanywa na Serikali. Hii inathibitishwa na ukweli kwamba barabara ya Uchira – Kisomachi iliyotengenezwa muda mfupi tu kabla ya kuanza kwa ujenzi wa LEKIDEA iliharibika na kusababisha kukwama kwa magari eneo la Mtemboni na Msufin. Eneo la Mbuyuni kwa Mtanzania lililorekebishwa na LEKIDEA limebaki kuwa salama. Hili ni jambo ambalo LEKIDEA inapaswa kujivunia. Mhandisi wa barabara (W) ameliona hili na wakandarasi wa barabara watatakiwa kuzingatia viwango pindi wafanyapo kazi katika eneo letu.

Wapendwa wana LEKIDEA
Serikali nayo haijawa mbali na juhudi zetu. Mtakumbuka kuwa miaka miwili iliyopita barabara ya Uchira – Kisomachi ilikuwa mbaya sana, Serikali ilitoa T.Shs.47,000,000/= kuirejesha mahali pake. Pia zilitolewa T.Shs.5,500,000/= kutengeneza barabara ya Madukani – Kolaria. Hapo majuzi Serikali imetoa tena T.Shs.46,550,000/= kwa mkandarasi JABEL INVESTMENT CO. LTD ya jijini Dar es Salaam. Shughuli hii ya ujenzi ipo katika hatua ya “mobilization”. Hatuna budi kujenga uhusiano naye atuhakikishie kazi nzuri na ya viwango! Naambatanisha BOQS kwa kazi hiyo. Wakati huo huo Serikali imetoa T.Shs.9,300,000/= kwa matengenezo ya barabara ya Nganjoni – Mabungo iliyopo kwenye Kata yetu. Napenda kuwajulisha kuwa kwa tathmini niliyofanya Kata yetu inapata fedha nyingi toka kwenye mfuko wa barabara kuliko Kata nyingi za Halmashauri ya Moshi! Zaidi ya hayo barabara ya Kisomachi – Nganjoni – Masaera (Kilema) imeingizwa Serikalini. Hii itatuwezesha kupanua uwezo wa soko la Kileuo badala ya kumtafuta mchawi.

Serikali imetoa T.Shs.55,000,000/= kwa ajili ya maendeleo ya Shule ya Sekondari Kilimani chini ya mpango wa TASAF kutokana na fungu hilo Shule imeweza kununua madawati 100, viti 100, kabati za kuhifadhi vifaa, kujenga madarasa mawili na vyoo vya wanafunzi. Hata hivyo, madarasa yamekamilika kwa shida na vyoo kujengwa bila mfumo wa maji kutokana na kamati ya usimamizi (Mero) kutowajibika ipasavyo. Kwa vyovyote vile udhaifu uliojitokeza unaanzia kwa wataalamu wachache wasiokuwa waadilifu ndani ya Halmashauri ya Moshi. Tunafuatilia tatizo hili kwa karibu.

Jengo la Zahanati ya Kileuo lililokuwa limeanza tangu mwaka 2007 na kuzuiliwa kwa miaka kadhaa kutokana na usimamizi duni wa Serikali ya Kijiji, mkakati wa ujenzi wa Zahanati umepata msukumo upya baada ya Serikali kutuma tena T.Shs.20,000,000/= kwa masharti mapya chini ya uangalizi wa Kata. Tunatarajia kukamilisha ujenzi mwaka huu na tayari tumeshaingiza Zahanati kwenye mpango wa huduma za Serikali. Zahanati ya Kileuo imekuwa kikwazo kikubwa kwa ujenzi wa Ofisi ya Kata.

Tumeendelea kuhamasisha bustani za miche ya kahawa kwa ajili ya wakulima wetu.

Msimu huu chama chetu cha (KNCU) kimeweza kuzalisha miche 15,000 na kusambaza kwa wakulima wetu. Bei ya mche mmoja ni shilingi 300. Miche mingi iitolewa kwa mkopo kutokana na hali mbaya kifedha. Wakulima kadhaa wameanza kunufaika na matunda ya miche bora ya kahawa ijapokuwa bei ya kahawa imeshuka kwenye soko la dunia.

Tatizo la ukosefu wa ajira kwa vijana wetu limekuwa kwa kiasi kikubwa na limeanza kutishia maisha ya watu katika eneo letu. Kwa zaidi ya mwezi mmoja sasa uongozi wa Kata umewakusanya na kuwaunganisha vijana katika vikundi vya watu kuanzia 10 hadi 25. Tumewafundisha namna ya kuandika katiba ya vikundi na kutengeneza andiko la miradi na hivi karibuni tumetuma maombi ya mikopo Serikalini ili vijana waweze kunufaika na fungu la Maendeleo ya Vijana. Kutokana na mkakati huu vijana wameweza kujitambua ndani ya jamii na wengine wameweza kunyoosheana vidole pale ilipobidi kufanya hivyo. Tunasubiri tuone mwisho wake.

Hapana shaka kuwa mikakati ya kimaendeleo iliyoanzishwa LEKIDEA imeleta changamoto mbalimbali katika historia ya maendeleo Kirua Vunjo. Kutokana changamoto hizi, zimejitokeza harakati mbalimbali ambazo zimeanza kukabili viongozi ambao wameshindwa kuendana na mahitaji ya sasa ya wanachi. Viongozi / Watumishi walevi, wazembe wsio waadilifu, wameanza kukumbana na kadhia hii. Tayari Mwenyekiti wa Kijiji cha Mrumeni amekumbwa na karaha hii. Wimbi linaendelea na hakuna anayejua mwisho wa siku litakuwaje. Cha msingi ni mabadiliko chanya.

Naomba nisiwachoche sana kwa mawazo yangu nikaribishe hoja mbalimbali kwa ajili ya kupambana na changamoto zetu za kimaendeleo katika eneo letu. Mungu aendelee kuwajalia afya na uzima.



Alex J. Umbella
DIWANI
Kata ya Kirua Vinjo Mashariki.
Aug 2013



Bil of Quantities for Uchira - Kisomachi Road - 7Km


Spesc




S/n
Eescription of Work
Ref
Unit
Qty
Rate
Amount
1
Part A.Preliminary ang General Items





1.1
Mobilization?Demobilization
1.2
Lsum
1
3,000,000.00
3,000,000.00
1.2
Provision sum for erection of sign






board
1.6
Lsum
1
6,000,000
6,000,000
1.3
Field compaction test and






laboratory material testing
1.5
Lsum
1
1,000,000
1,000,000

Sub Total Part . A




4,600,000







2.0
Part BOAD WORKS





2.1
Site clearance (grass cutting)
2.1
3000
300
900,000
2.2
Light reshaping
2.7.2
km
5
1,400,000
7,000,000
2.3
Excavate, Load, haul, spread,






water and compact gravel






wearing course 150mm think to






the required density (95%Mdd)
2.8
1350
22,000
29,700,000







3.0
Sub Total Part . B




37,600,000
3.1
Part C. Drainage Works






Repair head walls and disilting






of concrete pipe culverts 600mm






diameter
4.4
Nos
4
100,000
400,000
3.2
Re-excavate mitre drains
5.1.5
m
300
1,500
450,000

Construction of stone masonry






line ditches
5.14
m
70
50,000
3,500,000








Sub Total Part . C




4,350,000








GRAND TOTAL (A+B+C)




46,550,000

















































Bill of Quantities for Nganjoni - Mabungo Road 4.5km







S/n
Eescription of Work
Spesc Ref
Unit
Qty
Rate
Amount
1.0
Part A.Preliminary ang General Items





1.1
Mobilization / Demobilization
1.2
Lsum
1
1,000,000
1,000,000

Sub Total Part .A




1,000,000







2.0
Part B. ROAD WORKS





2.1
Site clearance (grass cutting)
2.1
1500
300
450,000
2.2
Light reshaping
2.7.2
KM
3.5
1,400,000
4,900,000
2.3
Sport graveling
2.3.3
50
17,000
859,000

Sub Total Part . B




6,200,000







3.0
Part C. Drainage Works





3.1
Re-excavate mitre drains
5.1.4
M
100
1500
150,000
3.2
Repair head walls and disilting
4.4
Nos
2
30,000
60,000

of concrete pipe culverts 600mm






diameter





3.3
Suplply and fix concrete pipe t






culvert including inlet and outlet






drains, 150mm thick concrete






sorroundings grade 20, stone






masonry headwall, wing wall and






sprons.






a. 600mm dia concrete culverts
5.3
m
7
270,000
1,890,000

Sub Total Part C.




2,100,000








GRAND TOTAL




9,300,000








GRAND TOTAL SUMMARY




1
PRELIMINARY AND GENERAL ITEMS
TSHS.

7,600,000
2
UCHIRA - KISOMACHI


TSHS.

41,950,000
3
KAWAWA - YAMU - NDUONI

TSHS.

7,850,000
4
UCHIRA - MIWALENI - KISANGESANGENI
TSHS.

10,340,000
5
NGANONI - MABUNGO


TSHS.

8,300,000

GRAND TOTAL SUMMARY

TSHS.

76,040,000








---------------------------------------------------------


MPANGO MKAKATI WA KATA 2010-2020

MPANGO MKAKATI WA MAENDELEO KATA KIRUA VUNJO MASHARIKI 2010 - 2020





SEKTA
LENGO
UTEKELEZAJI
MHUSIKA
VIASHIRIA






Kuinua kiwango cha maisha cha




wakazi wa Kata ya Kirua Vunjo




Mashariki ifikapo mwaka 2020.








UONGOZI
Jamii iweze kujisimamia yenyewe
> Kujenga uwezo wa:-
DIWANI /
>  Uwepo wa Viongozi wanaoelewa

kwa ajili ya maendeleo endelevu.

MKURUGENZI
    majukumu yao.


(i)  Viongozi wa Vijiji.






>   Watendaji / Watumishi wenye


(ii)  Watendaji wa Vijiji

     mipango kazi.


      na Kata.






>   Vikao vya Serikali ya Vijiji


(iii) Watumishi wa umma

    kufanyika kisheria.


     ngazi ya Vijiji na Kata.






>   Mikutano Mikuu ya Vijiji inafanyika.


(iv) Wenyeviti wa Vitongoji

    


      wamudu kutekeleza

>   Ushiriki wa wananchi katika Uongozi.


     majukumu yao ya kila




     siku.

>   Jamii inachangia maendeleo yao.







>  Kuhamasisha wananchi
AFISA MAENDELEO
>   Vikundi vya wafugaji, biashara ndogo,


    waweze kutambua haki
JAMII
     ndogo wakulima hasa vya Vijana.


    zao za msingi na kuwajibika




    ipasavyo.









>  Kuunda vikundi vidogo




    vidogo vya uzalishaji




    mali (IGAs)









>   Ujenzi wa Ofisi ya Kata
DIWANI /
>   Ofisi mpya.



MKURUGENZI




MTENDAJI (W)











SEKTA
LENGO
UTEKELEZAJI
MHUSIKA
VIASHIRIA


>   Kuunda upya Benki ya Akiba

>   Watu wanaoweka na


     na Mikopo

      kuchukua fedha.


     (Kirua Vunjo East SACCOS)






>   Mikopo ikiidhinishwa na




     kurejeshwa.





KILIMO NA
Kuboresha na kuimarisha
>   Kuanzisha na kuendeleza
DIWANI /
>   Uwezo wa bustani za
UFUGAJI
upatikanaji wa chakula katika
     mifereji ya asili kwa ajili
AFISA KILIMO
     mboga na ustawi

ngazi ya Kaya.
     ya umwagiliaji.

     wa mashamba ya




     uzalishaji mali


>   Kutoa mafunzo kwa wakulima

     yasiyotegemea mvua


     wadogowadogo Kuhusu mbinu bora

     kwa 100%.


     za uzalishaji.









>    Kujenga uhusiano hai kati ya

>   Upatikanaji wa aina


      maendeleo na watoto.

      mbalimbali za lishe, pia watoto




      kwa ridhaa yao wapewe nafasi




      ya kufuga wanyama wadogo wadogo




       kama - sungura, visili, kuku n.k.


>   Kuanzisha / Kuendeleza




     shughuli za uhifadhi wa ardhi




      na kuboresha vyanzo vya maji.

>   Uwepo wa bustani za




     miti, ili kutunza asili ya maeneo yetu.


>   Kuanzisha bustani mama na

>   Vyanzo vya maji vilivyo-


     kuendeleza bustani zilizopo

     pandwa miti.


     kukuzia miche bora ya kahawa.









>   Kuboresha mifugo m.f. ngombe,

>   Usambazaji wa miche


     mbuzi, kuku wa kienyeji na hata wa

     bora ya kahawa kwa


     kisasa.

     mkulima mmoja mmoja.









>   Kituo cha uhamilishaji




    









>   Upatikanaji wa mifugo




     bora.
SEKTA
LENGO
UTEKELEZAJI
MHUSIKA
VIASHIRIA





ULINZI NA
Ustawi wa Ulinzi na Usalama
>   Kuanzisha kikosi Kata cha
DIWANI /
>   Ufuatiliaji wa kudumu wa
USALAMA
wa raia na mali.
     wanamgambo kwa ajili ya
MTENDAJI KATA
     uhalifu.


     ulinzi na usalama wa raia na




     mali zao.









>   Kutoa mafunzo kwa kikosi cha

>   Uhalifu  kupungua.


     wanamgambo kwa kila Kijiji.









>   Kujenga dhana ya ufahamu

>   Mawasiliano chanya kati


     wa uhalifu baina ya raia.

     ya raia na Viongozi.







>   Kutengeneza mazingira ya kila

>   Upatikanaji wa sheria


     mwenye uwezo wa kufanya

     ndogondogo dhidi ya


     kazi awajibike ipasavyo.

     uzururaji, ulevi, matusi n.k



DIWANI



>   Ujenzi wa kituo cha Polisi na
LEKIDEA
>   Uwepo wa Kituo cha Polisi Kata


      Mahakama.
MKURUGENZI
     na Baraza la usuluhishaji.















SEKTA
LENGO
UTEKELEZAJI
MHUSIKA
VIASHIRIA





ELIMU
Kutoa elimu bora kwa watoto wa
>   Ujenzi wa miundombinu ya
DIWANI / MRATIBU
>   Kupungua kwa watoto

umri wa kwenda shule.
     kutosheleza k.v. madarasa, jiko,
ELIMU KATA
     wazururaji mitaani.


     stoo, vyoo na viwanja vya
AFISA ELIMU (W)



     michezo katika shule za msingi.

>   Mahudhurio kuongezeka.







>   Ujenzi wa miundombinu

>   Michezo kufanyika mashuleni.


     inayohitajika katika shule za




     sekondari k.v. madarasa, maktaba

>   Ufaulu wa shule za


     maabara, vyoo na nyumba za

      sekondari kuongezeka.


     walimu.






>   Upatikanaji wa vitabu,


>   Uzambazaji wa vifaa vya

     samani nyingine ambazo ni muhimili


      kufundishia katika shule za

     wa Elimu.


      msingi na sekondari.






>   Kiwango cha mahudhurio


>   Kuhamasisha walimu na

     ya walimu kuongezeka.


     kurejesha nidhamu ya kiutendaji









>   Kuhamasisha wazazi /

>   Upatikanaji wa chakula


     wananchi kutambua jukumu la

     cha mchana mashuleni.kufuta dhana


     kuchangia elimu.

      kwamba Elimu ni sehemu ya ukuaji




      kwa kuhamasisha jinsi ya kutumia




      utajiri wa fikra kuleta ukombozi wa




      maisha.










SEKTA
LENGO
UTEKELEZAJI
MHUSIKA
VIASHIRIA





AFYA
Kuinua kiwango cha afya ya
>   Kuhamasisha wanajamii kujenga
DIWANI
>   Ongezeko la vyoo bora.

msingi ya Jamii.
     vyoo bora katika kila Kaya.
AFISA AFYA








>   Kufanikisha zoezi la chanjo kwa

>   Takrimu za chanjo kuongezeka.


     watoto wa umri chini ya miaka mitano.









>   Ujenzi wa vituo vya tiba na upatikanaji

>   Uundaji wa kamati za afya


     wa dawa za tiba.

     zinazofanya kazi.







>   Kusimamia zoezi la usafi binafsi na  

>   Taarifa za ukaguzi.


     usafi wa mazingira majumbani.









>   Kusimamia zoezi la usafi wa maeneo

>   Ukaguzi wa vyanzo unafanyika


     umma k.v. mashuleni, vilabuni, sokoni,

     siku hadi siku.


     vituo vya tiba na machinjio.









>   Kuanzisha na kuendeleza michezo.

>   Vijana wanaojishughulisha na michezo




     kama moja ya burudani.















SEKTA
LENGO
UTEKELEZAJI
MHUSIKA
VIASHIRIA





UKIMWI
Kusia mbegu ya matumaini kwa
>   Kuunda kamati za UKIMWI ngazi za
AFISA MAENDELEO
>  Wagonjwa na waathirika

wagonjwa na waathirika wa
     Vijiji na Kata.
JAMII / DIWANI
     wanatembelewa.

UKIMWI na magonjwa sugu.

AFISA AFYA



>   Kuanzisha mfuko wa huduma kwa

>   Dawa, chakula, nguo vinatolewa


     wagonjwa na wanaoishi na virusi vya

     kwa wahusika.


     UKIMWI

>   Watoto waathirika / yatima wanalipiwa




     ada shuleni.







>   Waathirika wanawezeshwa kwa lengo

>   Miradi ya mbuzi wa maziwa.


     la kujitegemea.

>  Bustani za mbogamboga.




>   Ustawi wa biashara ndogondogo




     kwa waathirika.







>   Kutoa elimu kwa Jamii.

>   Mabadiliko ya tabia yenye kujenga




     amali na tunu bora za ukuaji na




     upambanaji dhidi ya mazingira




     hatarishi. Upendo kuelekezwa kwa




     wahanga wa moja kwa moja na




     wagonjwa.















SEKTA
LENGO
UTEKELEZAJI
MHUSIKA
VIASHIRIA





Mawasiliano
Kuboresha maendeleo ya
>   Ujenzi na upanuzi wa barabara za
DIWANI
>   Barabara zinapitika majira yote kwa
na Nishati
miundombinu ya mawasiliano na

LEKIDEA
     mwaka.

nishati
(i)   Uchira - Kisomachi - Kolaria.
MKURUGENZI





>   Upatikanaji wa usafiri mbadala.


(ii)  Kisomachi - KNCU - Kilasanioni.






>   Ongezeko la bidhaa na


(iii)  Kisomachi - Kiwelewe - Lasso.

      wafanyabiashara katika soko la




      Kileuo.


(iv)  KNCU - Sumi.









(v)   Kisomachi - Nganjoni - Masaera.









(vi)  Mabungo - Nganjoni - Legho Kilema.









(vii)  Kilasanioni - Kwamaambo - Iwa.









>   Kuboresha kiwango cha mitandao ya

>   Ujenzi wa minara ya mawasiliano .


     mawasiliano k.m. voda, airtel na tigo.






>   Mawasiliano angavu .


>   Ujenzi wa miundombinu ya nishati ya




     umeme.

>   Upatikanaji wa umeme Kileuo Kusini




     na Nganjoni.









>   Ongezeko la watumia  umeme.










NB. Umeandaliwa na Alex J. Umbella na kupitishwa na Kamati ya maendeleo ya Kata - K..V. mashariki


NOTE:
SEKRETARIAT YA LEKIDEA, BAADA YA KUVUTA PUMZI KIDOGO KUTOKANA NA MAJUKUMU MENGINE YA KIJAMII YALIYOKUWA HAYAEPUKIKI, HIVI KARIBUNI ITAENDELEZA TENA MAJUKUMU YAKE RASMI KWA SPEED NA UMAHIRI MKUBWA KAMA AWALI KUANZIA MWEZI UJA. KAMA TAARIFA ILIVYOKWISHATOLEWA NA MAKAMU-KATIBU WA LEKIDEA, NDG MARTIN M. KESSY.

TUNASONGA MBELE NA DAIMA TUTAFANIKIWA: TUUNGANE MIKONO.
Wenu;
SEKRETARIAT - LEKIDEA.