LEKIDEA FOCUS OVERVIEW

LEKIDEA
is a registered Non-profit Organization of Kirua Vunjo East Moshi, by Natives from related Villages (Kileuo, Mrumeni, Kotule, Mero, Legho, Lasso, Kwa-Laria(Kanji), dedicated to join together, leverage their Vision, Objectives, Social strengths, ambitions & professionalism and other common resources from members, relatives and families having any origination with K.V East, to come TOGETHER, DEVELOP and CHANGE their Motherland through Projects and involvements in different Social development Initiatives that play roles in alleviating poverty and enhancing opportunities in collaboration with all well wishers, and support from social development entities from the village level, national level, and international level.

LEKIDEA :: Matukio Mbali mbali pamoja na Picha

 Kikao Cha LEKIDEA, Tarehe 5/08/2011: Wajumbe wakiwa Katika kikao cha Uongozi na Sekretariet wakijadili na kuandaa mikakati ya Maendeleo ya Kirua Vunjo Mashariki chini ya LEKIDEA. Katibu wa LEKIDEA Ndg Joseph I. Shewiyo akiandika dondoo muhimu katika majadiliano hayo.

Kikao kikiendelea, wajumbe wanasikiliza kwa makini

Mjumbe - Ndg Baltazary Kissenga Assey akisisitiza jambo ikiwa ni katika maendeleo ya Kikao.

 Katibu - Ndg Joseph Shewiyo akisisitiza kuhusu suala wana-KV Mash. wote kuungana, katika maendeleo.

Wajumbe, kutoka kushoto, Ndg Paul Patrice Malyawere, Meku Nyange na Bernard Ndepachio Msacky wakisikiliza kwa makini maendeleo na Mikakati ya Miradi katika Kikao cha LEKIDEA.

Makamu M/Kiti, Ndg Eng. Simon T. Njau (wa tatu kushoto), akitoa maelekezo na ufafanuzi wa namna ya kuharakisha usanifu na usimamizi wa Mipango muhimu ya Mradi wa Barabara ya Uchira-Karumeli hadi Kwa-Laria.

Kikao kikiendelea, wajumbe na Katibu wanatafakari mikakati ya uhamasishaji wana-LEKIDEA

Mjumbe Ndg Meku Nyange akifafanua mikakati ya Uhamasishaji na ukusanyaji wa Michango ili kuharakisha ujenzi wa Barabara ya Uchira hadi Kwa-Laria, wakati wajumbe wote wakisikiliza kwa makini kabla ya kuchangia hoja na mawazo.

Mjumbe, Ngd Meku Nyange akiendelea kuelezea mikakati ya maendeleo

Makamu Katibu, Ngd Martin Mathias Kessy akinukuu maamuzi na maelekezo toka katika kikao cha LEKIDEA, wakati Wajumbe Wengine Ndg Emilian Joseph Saluo na Ndg Venance Vendelini Msacky wakifuatilia kwa umakini.

Kazi inaendelea, muda umeenda, usiku unazidi kwenda, wajumbe wameshajadili mambo muhimu, wamefikia hatua ya kuvuta pumzi kidogo, kuunganisha mawazo wakimsubiri Makamu Katibu akikokotoa makadirio na makusanyo.
Mjimbe, Mzee Apolinary Ndepachio, mshauri machachari akisisitiza agenda muhimu, wakati huo huo Mhazini Ndg Thomas Roman Msaky (wa pili kulia) akiendelea kukusanya Michango kwa ajili ya Miradi ya LEKIDEA.

Katibu wa LEKIDEA Ndg Joseph Shewiyo akisoma baadhi ya maamuzi ya Kikao cha LEKIDEA siku hiyo.

Mjumbe - Meku Nyange (wa pili kulia) akiwasiliana na wanachama wa LEKIDEA katika harakati za kuharakisha mikakati ya michango inasonga mbele

Baada ya Shughuli za Kikao kukaribia ukingoni, hapa wanaonekana wajumbe, (kutoka kushoto, waliokaa) Makamu M/Kiti, Ndg Martin M. Kessy akijipongeza kidogo kwa Pilsner baridi, wakati Mjumbe mwingine Ndg Venance V. Msacky , ambaye pia ndiye Mmiliki wa Double View Hotel, akicheka baada ya kutoa utani kidogo ikiwa ni hamasa ya maendeleo, na pembeni yake anaonekana Ndg Bernard Msacky akitabasamu
Baadhi ya Maeneoya Ukumbi wa Double View Hotel yakionekana baada ya Kikao cha Wana-LEKIDEA kukamilisha kikao chao.



-------------------------------&&&&&-----------------------------